Pages

Pages

Tuesday, August 01, 2017

Mkuu wa Mkoa Iringa akabidhi Milioni 20 za Biko kwa mshindi wao



*Ally Issa Kumburu naye akabidhiwa Mil 10 zake Dar es Salaam
Na Mwandishi Wetu, Iringa
MKUU wa Mkoa Iringa, Amina Masenza, jana ameshiriki kumkabidhi mshindi wa Sh Milioni 20 wa mjini Iringa, Viane Kundi, ambaye aliibuka na ushindi wa fedha hizo katika droo ya 27 iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Mkoa Iringa, Mheshimiwa Amina Masenza wa pili kutoka kulia akimkabidhi Sh Milioni 20 mshindi wa Biko droo ya 27, Viane Kundi wa mjini Iringa aliyeibuka kidedea Jumapili iliyopita. Wa kwanza kushoto ni Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles na kulia ni mtumishi wa NMB, Iringa,
Mshindi wa Biko wa Sh Milioni 20 Viane Kundi akifurahia fedha zake baada ya kukabidhiwa jana mjini Iringa katika benki ya NMB.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, RC Masenza alimpongeza mshindi huyo pamoja na kumtaka atumie fedha hizo kujikwamua kiuchumi kutokana na mamilioni hayo.
Alisema mchezo wa bahati nasibu ni moja ya sekta inayoweza kuinua uchumi wan chi endapo washindi watazitumia fedha zao kwa uangalifu, huku akiwahamasisha Watanzania, wakiwamo akina mama kucheza kwa wingi.

“Biko ni mchezo mzuri hata mimi nitaanza kucheza, hivyo naomba Watanzania wote tucheze Biko ili tuweze kuibuka na zawadi mbalimbali za Biko, ukizingatia kuwa pesa hizi zitakuwa mwangaza kwa washindi wote,” Alisema.
Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko kutoka mkoani Iringa, Viane Kundi akiwa na mume wake pamoja na mtoto wao wakifurahia donge nono la Biko baada ya kukabidhiwa katika benki ya NMB Mkoani Iringa.
Naye Mshindi wa droo maalum ya Komaa Concert ya Sh Milioni 10, Ally Issa Kumburu jana alikabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB, tawi la Bank House, Posta, jijini Dar es Salaam. Kumburu ni mkazi wa Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Mheshimiwa Paulo Makonda wa pili kutoka kushoto akipiga picha ya pamoja kwenye zulia jekundu baada ya kuwasili katika Tamasha la Komaa Concert mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe na kudhaminiwa na Biko. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe wa pili kutoka kulia, Mkurugenzi wa Biko, Charles Mgeta kushoto na Sadick Elimusu, Meneja Udhibiti wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania. Picha na Mpigapicha wetu.

Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema Biko ni mchezo unaotoa ushindi kwa kiasi kikubwa kwa washindi wake kuzoa zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja inayoingia kwenye simu ya mshindi dakika chache baada ya kushinda.

“Bahati nasibu yetu inachezwa kwa njia ya ujumbe wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo namba ya kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema.

Naye Viane mshindi wa Biko Milioni 20 Iringa, aliishukuru Biko, huku akisema fedha zake ataziingiza kwenye biashara ili ziweze kukuza uchumi wake, ukizingatia kuwa ndio kusudio lake kuu kuingia kwenye michezo ya kubahatisha.

“Nitafanya biashara kama sehemu ya kutimiza ndoto zangu kwakuwa tangu mwanzo nilikuwa namuomba Mungu niweze kushinda donge nono la Biko,” Alisema.
Katika hatua nyingine, mshindi wa droo maalum  ya Komaa Concert iliyofanyika jana, Ally Issa Kumburu, naye alikabidhiwa Sh Milioni 10 zake alizoshinda katika tamasha la burudani lililodhamiwa na Biko.
“Nashukuru kwa kukabidhiwa fedha zangu leo jijini Dar es Salaam, katika tawi la benki ya NMB, ambapo ndio nimeamini kuwa nimeshinda, ukizingatia kuwa watu tulikuwa wengi na kila mtu alitaka ashinde,” Alisema huku akishuhudiwa na Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven.
Heaven aliwakumbusha Watanzania kuendelea kucheza Biko ili wajivunie zawadi za papo kwa hapo pamoja na Sh Milioni 20 zinazotoka katika droo ya Jumatano na Jumapili.


No comments:

Post a Comment