Pages

Pages

Sunday, July 30, 2017

Viane Kundi wa Iringa ajishindia Milioni 20 za Biko


*Issa naye achota Mil 10 zake
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BAHATI Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ imezidi kushika kasi baada ya droo yake ya 27 kutua kwa Viane Kundi wa mjini Iringa, nchini Tanzania aliyevuna jumla ya Sh Milioni 20, huku Ally Issa Kumburu mkazi wa Mwananyamala, jijini Dar es Salaam naye akivuna Sh Milioni 10 za Tamasha la Komaa Concert, lililofanyika jana na kudhaminiwa kwa kiasi kikubwa na Biko. 
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, kushoto akiandika dondoo katika droo ya Komaa Concert iliyorudiwa leo asubuhi baada ya jana kutopaatikana mshindi katika Tamasha la Komaa lililoandaliwa na EFM Radio na kudhaminiwa na Bahati Nasibu ya Biko Tanzania. Kulia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, kushoto akiandika dondoo katika droo ya 27 ya Biko ambapo Viane Kundi wa Iringa, alitangazwa mshindi na kuzoa Sh Milioni 20 za Biko. Kulia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Paulo Makonda, akizungumza na wadau wa muziki waliofurika katika Tamasha la Komaa Concert lililoandaliwa na EFM Radio kwa udhamini mkubwa wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku'. Katika Tamasha hilo lililokwenda na kumpata mshindi wa Sh Milioni 10 limempata Ally Issa Kumburu wa Mwananyamala, aliyepatikana katika droo iliyochezeshwa leo baada ya ndani ya tamasha kutopokea simu kutokana na wingi wa watu na kelele za uwanjani Tanganyika Packers, Kawe. Mwingine pichani ni Mkurugenzi wa EFM Radio, Denis Busurwa (Sebo). Picha na Mpigapicha Wetu.
Msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Dogo Aslay, pichani akiwachezesha mashabiki wake waliofurika katika Tamasha la Komaa Concert lililoandaliwa na EFM Radio kwa udhamini mkubwa wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku'. Katika Tamasha hilo lililokwenda na kumpata mshindi wa Sh Milioni limempata Ally Issa Kumburu wa Mwananyamala, aliyepatikana katika droo iliyochezeshwa jana baada ya ndani ya tamasha kutopokea simu kutokana na wingi wa watu na kelele za uwanjani Tanganyika Packers, Kawe.

Droo zote mbili zilichezeshwa leo jijini Dar es Salaam kwa kuendeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, ambapo ni matokeo ya kutopatikana kwa mshindi wa tamasha la Komaa Concert, lililofanyika juzi katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika droo hiyo ya 27, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kupatikana kwa washindi hao ni sehemu ya kuendelea kugawa fedha kwa kwa wote wanaoshinda katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, akiwamo Kumburu wa Komaa Concert, mkazi wa Mwananyamala, jijini Dar es Salaam na Viane aliyejinyakulia Sh Milioni 20 akitokea mkoani Iringa.

Alisema Viane amekuwa mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya 27, ambapo anakuwa mmoja kati ya washindi wengi wanaojichotea zawadi nono ya Sh Milioni 20 kutoka Biko kwa droo ya Jumapili na Jumatano, pamoja na zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazolipwa moja kwa moja kwenye simu za washiriki wao, huku akiwataka Watanzania wacheze mara nyingi zaidi ili wajiwekee nafasi nzuri za kushinda zawadi za papo kwa hapo pamoja Milioni 20 kwa droo ya Jumatano na Jumapili.

“Jinsi ya kushinda Biko ni rahisi kwa sababu mshiriki anapaswa kufanya muamala kwenye simu yake kama vile Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo ataweka Sh 1,000 na kuendelea, huku namba yetu ya Kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema Heaven na kuwataka Watanzania kuendelea kucheza Biko ili waibuke na ushindi.

Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, alisema washindi wote wawili wamepatikana kwa kupigiwa simu, huku akisema kuwa droo ya Tamasha la Komaa Concert imerudiwa ili kujenga uhalisia, baada ya washindi wote wa jana kutopokea simu.

“Bodi yetu ipo makini kufuatilia michezo hii ya kubahatisha, hivyo tunawapongeza washindi wote wawili wa Komaa Concert ambaye ni Kumburu wa Mwananyamala pamoja na binti wa Iringa, anayejulikana kama Viane ambaye naye ameingia kwenye orodha ya washindi wa mamilioni ya Biko,” Alisema.

Kwa kutangazwa washindi wa Biko, Watanzania hao wenye bahati wanatarajiwa kukabidhiwa fedha zao mapema wiki ijayo, ikiwa ni mwelekeo wa Biko kutoa mamilioni ya fedha kwa washindi wao, huku kwa mwezi Mei na Juni pekee ikitoa zaidi ya Sh Bilioni moja kwa washindi mbalimbali wa bahati nasibu yao.

No comments:

Post a Comment