Pages

Pages

Wednesday, July 19, 2017

Milioni 20 za Biko zakimbiza homa ya Marianus wa Chanika


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
ZAWADI nono ya Sh Milioni 20 zinazotolewa na Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, zimekimbiza homa ya mshindi wa droo ya 24 ya Biko, iliyotangazwa leo jijini Dar es Salaam, huku akiipata mkazi wa Chanika, jijini Dar es Salaam, Enos Marianus.
Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akizungumza kwa simu na mshindi wa droo ya 24 ya Biko , Enos Marianus, aliyejizolea jumla ya Sh Milioni 20 atakazokabidhiwa haraka wiki hii. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed, akiandika dondoo za mshindi huyo wakati anazungumza kwa njia ya simu mara baada ya namba yake kuibuka kidedea katika droo hiyo ya 24. Picha na Mpigapicha Wetu.

Akizungumza kwa njia ya simu wakati anapewa taarifa za ushindi wake na Balozi wa Biko, Kajala Masanja, Marianus alisema kwamba amekuwa mchezaji mzuri wa Biko, huku habari za ushindi wake zikiikimbiza homa iliyokuwa inamsumbua kwa wiki moja sasa.

Marianus alisema kwamba ushindi wa Sh Milioni 20 aliyotangazwa na Biko utakuwa muafaka kwake kutokana na kujihusisha na biashara ndogo ndogo kwa ajili ya kusukuma mbele gudurumu la maisha yake.

“Nashukuru sana kwa kunitangaza mimi kuwa ni mshindi wa droo ya 24 ya Biko, hivyo hapa hata homa inayonisumbua imeondoka na nimepona kabisa kwa sababu ya habari zenu nzuri, nikiamini kwamba nikipata fedha hizo nitapiga hatua kubwa kiuchumi hususan katika biashara zangu,” Alisema Marianus.

Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba droo ya Jumatano imekwenda kwa mfanyabiashara mdogo wa Chanika, huku akiwataka wengine waendelee kucheza kwa ajili ya kuvuna donge nono la Sh Milioni 20 kwa Jumatano na Jumapili, pamoja na zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.

“Biko ni mchezo rahisi kushinda na unaweza kubadilisha maisha ya Watanzania, hivyo endeleeni kucheza kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kuanzia Sh 1,000 na kuendelea, huku kiasi cha fedha cha Sh 1000 kikitoa nafasi mbili za ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa za Sh Milioni 20 za Jumatano na Jumapili, namba ya kampuni ikiwa ni 505050 na kumbukumbu ni 2456,” Alisema.
Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania,  Abdallah Hemed, alisema mchezo wa Biko unachezeshwa kwa kufuata sheria zote za michezo ya kubahatisha, huku akiwataka Watanzania kuuamini na kutumia fursa za ushindi kwa ajili ya maisha yao.

Biko ni mchezo wa kubahatisha unaotikisa katika viunga mbalimbali vya Tanzania, huku mwezi Mei na Juni pekee ukitoa zaidi ya Sh Bilioni moja kwa washindi wake walioshinda zawadi mbalimbali kutoka kwenye bahati nasibu hiyo, huku mshindi wa droo ya 24 akitarajiwa kukabidhiwa fedha zake haraka iwezekanavyo.


No comments:

Post a Comment