Pages

Pages

Monday, July 17, 2017

Biko yashauri washindi wake wafanye vitu vya maendeleo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 
WITO umetolewa kwa washindi wa bahati nasibu ya Biko wanaoendelea kupatikana kila siku wafanye vitu vya maendeleo mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao za fedha kutoka kwenye bahati nasibu hiyo ya aina yake.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, kulia akimkabidhi kiasi cha Sh Milioni 20 mshindi wao Fredy Nyari wa Kigamboni aliyeibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 katika droo ya 23 juzi. Kushoto ni Afisa wa NMB.

Hayo yamesemwa na Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alipokuwa anamkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wa Jumadili (Jumapili), Fredy Nyari, akiwa ni mshindi wa droo ya 23 ya Biko.

Akizungumzia hatua ya makabidhiano ya fedha hizo, Heaven, alisema kwamba ikiwa siku zote mtu anakosa mtaji wa kuanzisha au kuendeleza biashara zake, kupata Milioni 20 kwa mara moja si jambo la mzaha.

Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko droo ya 23, Fredy Nyari, akiwa na uso wa furaha baada ya kukabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kulia akiwa na mshindi wao wa Sh Milioni 20 Fredy Nyari baada ya kumkabidhi fedha zake katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam leo mchana. 
Alisema ni wakati wao sasa washindi wote wa Biko wale wanaopata zawadi nono ya Sh Milioni 20 inayotoka kila Jumatano na Jumapili pamoja na zawadi za papo kwa hapo zinazoanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja wanakuza uchumi wao.

“Kwa kuanzia Sh 1,000 tu mtu anaweza kushinda 5,000 hadi Milioni 20 kwa droo zetu kubwa, ambapo ni rai yetu kwa washindi wote kuwataka maisha yao yabadilike kwa kutumia vyema fedha zao baada ya kucheza Biko, mchezo unaochezwa kwa kufanya miamala kwenye simu za TIGO Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo namba yetu ya Kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema Heaven.

Naye Nyari, mshindi huyo wa droo ya 23 aliyotangazwa juzi jijini Dar es Salaam, alisema ni jambo la kumshukuru Mungu kwa hatua yake ya kuibuka na ushindi wa Sh Milioni 20 uliokuja kuyabadili maisha yake baada ya kukabidhiwa jana katika Tawi la Benki ya NMB, jijini Dar es Salaam.

“Wakati napigiwa simu ya ushindi na balozi wa Biko, Kajala Masanja, hakika nilikuwa siamini, ukizingatia kuwa wanaocheza Biko ni wengi na kila mtu anataka yeye awe mshindi wa Jumatano au Jumapili, hivyo kwangu mamilioni haya niliyokabidhiwa leo yamekuja kunibadilisha kwa hatua moja kwenda nyingine.

“Nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kwamba napiga hatua kubwa, ili pamoja na mambo mengine, niweze kutimiza ndoto zangu na kuwaaminisha waendeshaji wa mchezo wa Biko kuwa fedha zao zinabadilisha maisha yangu kiuchumi,” Alisema.

Moja ya sifa kubwa ya bahati nasibu ya Biko ni kitendo chake cha kuwakabidhi washindi wao fedha zao wanazoshinda siku moja tu baada ya kutangazwa washindi jambo linaloongeza chachu ya kupiga hatua kimaendeleo, huku kwa kipindi cha mwezi Mei na Juni pekee, wakiweza kuwapa washindi wao zaidi ya Sh Bilioni moja tangu kuanzishwa kwa bahati nasibu yao.
                                                 


No comments:

Post a Comment