Pages

Pages

Wednesday, November 02, 2016

Baraza la Madiwani Ileje labariki kufutwa kazi kwa watumishi wawili

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje, Haji Mnasi akiongea wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.

Na Fredy Mgunda, Ileje
BARAZA la Madiwani Wilayani Ileje limebariki kufutwa kazi kwa watumishi wawili wa Halmashauri hiyo kutokanana makosa ya wizi wa mamillioni ya fedha za wafadhili za mradi wa UKIMWI wa water reed.

Akizungumza wakati wa kufungwa kwa Baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Ubatizo Songa amesema kuwa, wameamua kuchukua uamuzi huo mara baada ya kuridhishwa na uchunguzi uliofanywa na kamati ya uchunguzi iliyoundwa na Ras wa Songwe na kubaini kuwa, Mganga Daraja la pili Josephat Yisuya na Grace Kibona wameweza kuingizia Halamashauri hasara ya zaidi Milioni 84.

“Josephati aliweza kujipatia kiasi cha fedha shilingi milioni 36254200 /-wakati Grace Kibona Mhasibu Daraja la kwanza aliweza kujipatia Kiasi cha shilingi milioni 48742500/-fedha za mradi wa Water Aid zilizofika katika Halmashauri ya wilaya ya Ileje,”alisema Songa.
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la madiwani Wilaya ya Ileje. 



Mwenyekiti huyo ameagiza watu hao kurudisha kiasi hicho chote cha Fedha katika Akaunti ya Halmashauri hili ziweze kufanya kazi zingine.
 
kwa mtumishi mwengine Anna mwakipesile kesi yake bado inaendelea na uchunguzi wakati huo watumishi 2 baada ya kamati ya uchunguzi iliyoundwa na ras songwe waliachiwa huru na kurudishwa kazini baada ya tume kuridhika na utetezi wao


Wakati huo huo Mkurugenzi mtendaji Bw Haji Mnasi amewavua vyeo wakuu wa shule wawili ambao ni Henry Musomba wa sekondari Ibaba na Emecka Minga wa sekondari Ngulugulu kwa makosa mabalimbali yakiwemo utoro,uzembe ,lugha chafu na matumizi mabaya ralislimali

Aidha Mnasi alisema kuwa ni wakati wa kila mfanyakazi wa serikalini kujitathimni kwa kile alichofanya kwani waliotuhumiwa ni wengi lakini bado uchunguzi unaendelea hivyo hawajaishia hapo kwani kila mmoja atakayebainika kufanya ubadhilifu sheria itafata mkondo wake.

Ametoa onyo kwa watumishi kuacha kujihusiha na mambo yaliyo kinyume na maadili ya utumishi wa kwa kujiingiza katika masuala ya kifisadi serikali aitamfumbiamcaho kwani hu ni wakatii wa kuwahudumia wananchi wa nyonge kwa maslahii ya Taifa.

“Mimi sipo tayari kufukuzwa kazi kwa uzembe wa watumishi wazembe nitafuatili utendaji wa watumishi wote wa Ileje ili tuweze kuwatumikia wananchi kama inavyopaswa na kuidumisha kauli ya hapa kazi tu iliyotelwa na rais wetu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Dr John Pombe Magufuli” alisema Mnasi

No comments:

Post a Comment