Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, pichani.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Taasisi inayoongoza Tanzania kwa kubobea katika kutoa mikopo nafuu, Bayport Financial Services katika kipindi cha miaka 10 iliyopita imechangia kwa kiwango kikubwa katika kuboresha maisha ya maelfu ya Watanzania kupitia utoaji wa mikopo.
Bayport Tanzania ni miongoni mwa taasisi tanzu kumi za Taasisi ya Bayport Group ambayo hutoa ufumbuzi wa kifedha kwa watu binafsi walioko katika ajira rasmi au waliojiajiri ndani ya soko linaloibukia. Huduma zinazotolewa na taasisi hiyo zinaboresha ujumuishwaji kifedha kwa watu ambao hawana uwezo wa kuzifikia huduma za kawaida za kibenki au walio na kiasi kidogo cha fedha katika benki.
Baada ya kuanza shughuli zake nchini Zambia mwaka 2001, shughuli za Bayport kwa hivi sasa zinaendeshwa katika nchi saba barani Afrika na nchi mbili ndani ya Amerika Kusini. Nchi hizo ni Zambia, Uganda, Ghana, Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Msumbiji, Colombia, na Mexico.
Hivi sasa Bayport imekuwa ni msingi wa kuaminiwa na mteja ikiwa na takribani wateja 518,000 ambao kila mara wamekuwa wakipata na hata na kufurahia huduma inazozitoa.
Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga, Bayport imeshatoa zaidi ya shilingi bilioni 48 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015 peke yake. Kwa upande mwingine Bayport inachukuliwa kuwa ni ‘mlipa kodi mkubwa’ nchini Tanzania ikiwa imelipa zaidi ya shilingi bilioni 7 kwa mwaka wa fedha 2014.