Pages

Pages

Wednesday, October 12, 2016

Msajili wa vyama vya siasa amuumbua Julius Mtatiro

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Msajili wa Vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi, amesisitiza kwamba ana mtambua Prof. Ibrahim Lipumba kama mwenyekiti halali wa chama hicho na Maalim Seif Sharrif Hamad kama katibu mkuu wa chama hicho.
''Mtatiro yeye ni nani, na ananipa Onyo kama Nani?, Ofisi ya Msajili inaitambua CUF moja tu, CUF ambayo mwenyekiti wake ni Lipumba na Katibu Mkuu wake ni Maalim Seif, Mtatiro hana mamlaka yoyote katika CUF kisheria hivyo asiendelee kuwapigia kelele''. alinukuliwa Msajili Mutungi.
''Chama cha siasa hakiwezi kuwa na uongozi wa aina mbili, yaani uongozi wa mwenyekiti Lipumba na Uongozi wa Mwenyekiti Mtatiro, hilo kwangu halitambuliki na halitakaa litambulike, lazima CUF waheshimu sheria za Nchi''. aliongeza Jaji Mutungi.
Kadharilka Msajili huyo amesema kwa sasa anaiona Bodi ya Wadhamini ya Chama hicho ikiwa imegawanyika makundi mawili, kundi linalomuunga mkono Lipumba na lile linalomuunga mkono Maalim.
''Anasema wadhamini, lakini anaonyesha wadhamini wawili tu, mwenyekiti na katibu, Bodi ya wadhamini ya CUF ni zaidi ya Mwenyekiti na Katibu, wapo wengine, na kwa kweli wamegawanyika kati kati wengine wameleta maombi haya, na wengine wameleta maombi yale, ofisi yangu haiwezi kuendeshwa na watu wa aina ya kina Mtatiro''. aliongeza
''Angewaambia waliosajiliwa Rita ni wangapi na hapo anao wangapi na msimamo wa wengine ni upi?, Ofisi yangu inawaheshimu wote 8 na haiwezi kufanya maamuzi kwa matakwa ya wajumbe wawili au watatu''. aliongeza
Aidha Msajili alisisitiza kuwa Ofisi yake ina wajibu wa kuhakikisha inasimamia fedha za umma ambazo zinatolewa kama ruzuku na kuhakikisha zinawafikia watu salama.
''Ruzuku ya CUF ipo salama na itaendelea kuwa Salama, walichoomba kina Lipumba ni kutambulishwa kama viongozi halali wa chama chao ili waweze kufungua akaunti, wala Msajili hajawatuma wakafungue akaunti ya Ruzuku, matumizi ya akaunti wanayajua waliofungua wenyewe''.. alisisitiza Msajili Mutungi.

No comments:

Post a Comment