Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed, katikati akimkabidhi hati mteja wao Mary Simon, baada ya kukamilisha taratibu za kupata kiwanja cha Vikuruti, vilivyopo Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Viwanja hivyo vinapatikana kwa njia ya fedha taslimu na mikopo maalumu kwa watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali. Kulia ni Meneja Mikopo wa taasisi hiyo, Nasibu Kamanda. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services, jana imeendeleza utaratibu wake wa kugawa hati kwa wateja wao walionunua viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani kwa njia ya mikopo na fedha taslimu.
Mradi huo wa Vikuruti ulizinduliwa mwaka jana, ambapo baada ya kufanikiwa kwake, taasisi hiyo ikaanzisha miradi mingine mitano ambayo ni Kigamboni, Bagamoyo, Chalinze, Kibaha na Kilwa, huku ikiweka utaratibu rahisi na nafuu.
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed, katikati akizungumza jambo baada ya kumkabidhi hati mteja wao Mary Simon kushoto baada ya kukamilisha taratibu za kupata kiwanja cha Vikuruti, vilivyopo Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Kulia ni Meneja Mikopo wa Bayport Financial Services, Nasibu Kamanda.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed, alisema kwamba kugawa hati kwa wateja wao ni mwendelezo wa huduma nzuri zinazotolewa na taasisi yao kwa ajili ya kuwakomboa wananchi katika suala zima la ardhi.
Alisema kwamba makubaliano yao ni kuhakikisha taasisi inasimamia sualaa la hati ili wateja wao wasisumbuke kutokana na mchakato mzima wa utendaji kazi wao unaotoa urahisi juu ya upatikanaji wa viwanja vyao vyenye hati.
“Tunaendelea na kutoa hati kwa wetu walionunua viwanja vya Bayport vilivyopo Vikuruti, ambapo Watanzania wengi walichangamkia fursa ya upatikanaji wa viwanja hivyo, ambavyo ukiacha vya Vikuruti, wateja wetu pia wanaweza kukopa fursa hii ya ardhi kwa miradi yetu ya Kimara Ng’ombe (Bagamoyo), Msakasa (Kilwa), Tundi Songani (Kigamboni), Boko Timiza (Kibaha), Kibiki na Mpera
Pages
▼
Pages
▼
Tuesday, August 23, 2016
Thursday, August 11, 2016
Uongozi wa shule za FEZA wasema hawafungi shule zao ng'o
Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
UONGOZI wa Shule za Feza nchini umeibuka
na kukanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii, kuwa wao
hawana uhusiano na Fethullah
Gulen wala serikali ya Uturuki kwa
vile hawajawahi kupokea misaada toka
pande hizo mbili za uendeshaji na kuwa shule hizo hazitafungwa.
Kauli hiyo imetolewa baada ya hivi karibuni kuenea kwa uvumi kuwa shule
za Feza zipo hatarini kufungwa kwa madai
kuwa mmiliki wake ni yule aliyejihusisha na jaribio la kuipindua serikani nchini Uturuki.
Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hizo, Habibu Miradji aliyasema hayo alipokuwa
akizungumza na wanahabari Kawe jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Alisema Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa shule za Feza ni kama
asasi zingine zilizosajiliwa kisheria na
serikali, hivyo ni mali ya watanzania.
“Shule za Feza zitabaki kuwa kiwanda
cha kuzalisha wazalendo wa kitanzania
na raia bora wa duniani, hivyo wazazi wanapaswa kuondoa hofu,” alisema.
Alisema toka mwaka 1995 shule hiyo imepata mafanikio ya kujenga shule za
awali tatu, shule za msingi mbili, sekondari tatu na shule ya kimataifa moja.
Aliongeza kuwa huo ni
uwekezaji wenye mchango katika kukuza
pato la taifa, kutoka awamu ya pili, tatu, nne hadi awamu ya tano chini ya Rais
John Magufuli.
\Alisema shule ya Feza ni hazina kwa Tanzania kwani shule zake
zimekuwa zikishika nafasi ya 10 bora toka mwaka 2004 hadi leo.
Alisema
wanatoa wito kwa wazazi kuwasiliana na uongozi wa shule hiyo kujua kinachoendelea kwenye shule husika kwa
manufaa ya wanafunzi wetu na taifa bila kusikiliza uvumi huo unaoenezwa na watu wasiopenda maendeleo ya shule hizo.
Mgodi wa BUZWAGI wakabidhi hundi ya sh milioni 700 Halmashauri ya mji Kahama
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo akizungumza katika
hafla ya kukabidhi hundi ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya mji wa
Kahama, hafla hiyo ilifanyika baada ya kukamilika kwa hafla ya kukabidhi
madarasa ya shule ya
msingi Budushi na nyumba za walimu Mwime.
Na Dixo Busagaga wa Michuzi Blog, Kanda ya Kaskazini.
Mgodi wa Buzwagi umekabidhi halmashauri ya mji wa Kahama hundi yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia saba na kumi na saba (717,276,055/=) ikiwa ni sehemu ya malipo ya kodi ya huduma(service levy) ambayo hulipwa kwa halmashauri hiyo.
Akizungumzia malipo hayo ya hundi Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo amesema kiasi hicho ni malipo ya kuanzia mwezi januari hadi juni mwaka huu.
Mwaipopo ameongeza kuwa licha ya Kampuni yake kulipa kodi mbalimbali na kujishughulisha katika kufadhili miradi ya Maendeleo, amesema ipo haja ya Jamii kuilinda na kuitunza miradi hiyo ili iwe na manufaa kwa Jamii nzima.
Uharibifu wa miundo mbinu ya vituo vya mabasi ya mwendo kasi ni tatizo
Fredy Njeje, Dar es Salaam
Ikiwa ni takribani miezi michache kupita tangia mabasi ya mwendo kasi yaanze kufanya kazi kwa ufanisi mzuri, kumekuwa na mambo kadha wa kadha yakiendelea ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa miundombinu ya vituo hivyo vya mabasi hayo.
Hili limeonekana bila chenga Morogoro Road ambapo kipande cha kutokea Jangwani mpaka Manzese kikionesha wazi vifaa vya kuhifadhia taka vimeharibika, huku vingine vikionekana kuchomolewa, kupinda na kulegea.
Swali la kujiuliza hapa ni kwamba kwa jinsi miundombinu hii ilivyo kaa ni ngumu sana hata mtu kugonga kwa mguu sasa inakuwaje inaharibika kiasi hiki?
Hapa upande wa kulia ukionekana kuwa kifaa cha kuhifadhia taka kilisha chomolewa na kubakiza mfuniko tuu na papo hivi kwa zaidi ya mwezi sasa.
Hapa Kifaa cha kuhifadhia taka taka kikiwa kimepinda haijulikani kiligongwa au kuna watu walikuwa wanataka chomoa.
Hiki kikiwa kimelegea kabisa amambapo muda wowote litachomoka
Hapa mfuniko ndio ulisha potea tena
Hili nalo tayari linaelekea kudondoshwa chini
Hii hapa ndio funga kazi kabisa yani wamesha chomoa muundo mbinu wote wa kushoto.
Wadhamini wa urembo warudisha hadhi ya shindano la Miss Tanga 2016
Miss Tanga 2016, Eligiva Mwasha
akiwapungia mikono wananchi waliojitokeza kushuhudia shindano hilo mara
baada ya kutangazwa kuwa mshindi.
Miss Tanga 2016, Eligiva Mwasha akiwapungia mikono watazamaji waliojitokeza akiwa na mshindi wa pili na tatu katika Shindano hilo ambalo liliandaliwa na Radio Tanga Kunani (TK) na Hotel ya Tanga Beach Resort.
Na Oscar Assenga, Tanga
WAKATI shindano la kumsaka malkia wa Mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016)likifanyika mwishoni mwa wiki na hatimaye mrembo Eligiva Mwasha kuibuka na ushindi kwenye kinyang’anyiro hicho dhidi ya washiriki wengine 10.
Shindano hilo ambalo lilisimama kwa muda baada ya serikali
kulisimamisha lile la Taifa msimu huu lilionekana kuwa na msisimuko wa hali ya juu kuanzia wapenzi,wadau na washiriki iliyochangiwa na waratibu wa shindano hilo Radio ya Tanga Kunani FM (TK) wakishirikiana na Hotel ya Tanga Beach Resort.
Ushindani wa washiriki hao ulianza kuonekana tokea wakati warembo hao wakiwa kwenye kambi yao ambayo ilifanyika kwenye hotel hiyo ambapo kila mmoja alionekana kuwa na shauku kubwa ya kutaka kuondoka na taji hilo.

Wednesday, August 10, 2016
Mgodi wa BUZWAGI wakabidhi shule wilayani Kahama
Kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart yanyakua tuzo Kimataifa
Mwenyekiti wa Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart, Yono Kevela, akionesha tuzo za kimataifa ya ufanisi bora wa kazi baada ya kukabidhiwa.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Udalali ya Yono Auction Mart, imekabidhiwa tuzo ya Mshindi wa Kimataifa ya Ufanisi na Ubora wa Kazi, baada ya kushindanishwa na kampuni nyingine 49 za nchi tofauti duniani hatua iliyotokana na utendaji wake katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza Jijini Dar es salaam jana, Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Yono Kevela, alisema ushindi huo unatokana na ufanisi wao wa kazi zikiwepo za ukusanyaji madeni ya kodi kutoka kwa wadaiwa sugu wa serikali .
Kevela alisema baadhi ya kazi walizofanya baada ya kupata zabuni ya kukusanya madeni ya wadaiwa ni za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wizara mbalimbali, taasisi za fedha na wakala wa serikali pamoja na wadau wengine.
Alisema ushindi wa tuzo hiyo ni faida ya ufanisi wa kazi zao katika kukusanya kodi za serikali huku akiahidi kutobweteka katika jukumu hilo alilopewa na Serikali hadi kushinda tuzo hiyo na badala yake atazidi kuongeza juhudi ili kampuni hiyo izidi kufanya vizuri.
“Tunashukuru kazi na huduma zetu kutambuliwa kimataifa, tumekuwa mabalozi wazuri wa Tanzania, tumetumia fursa hiyo kuitangaza nchi na kuwahimiza wawekezaji kuja kuwekeza “, alisema. Kevela
Alisema Tuzo hiyo ilitolewa Ufaransa na sherehe za kukabidhi washindi tuzo hizo zilifanywa Juni 25, mwaka huu Rome Italia ambako kampuni hiyo imeshinda ikitoka sekta binafsi, huku upande wa serikali ukishinda sekta ya Utalii kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Kampuni hiyo ya Yono imejizolea umaharufu hivi karibuni bada ya kupewa kazi ya kukusanya madeni ya wadaiwa 24 wa TRA, yenye thamani ya Sh bilioni 18.95 baada ya wadeni hao kutorosha kontena za mizigo yao kwenye Bandari Kavu (ICD) ya Azam mwishoni mwa mwaka jana.
Hata hivyo baada ya kampuni hiyo kuanza kazi, baadhi ya wadaiwa walifanikiwa kulipa madeni yao huku wengine wakilipa kiasi na wengine mali zao walikubali zikamatwe na kuuzwa ili kulipa madeni hayo, ambapo hadi sasa zaidi ya Sh bilioni saba zimeshakusanywa.
Maeneo mengine ambayo kampuni hiyo inafanya kazi ya kukusanya madeni dhidi ya wadaiwa mbalimbali ni pamoja na maeneo ya ardhi, mahakama, mabenki na taasisi zingine.
Monday, August 08, 2016
Tigo nao watamba maonyesho ya nane nane
Salasala sasa yapata mwarobaini wa maji
Meneja wa mkoa wa Dawasco -Tegeta Alpha Ambokile akizungumza na wakazi wa mtaa wa Upendo Salasala jijini Dar es Salaam ambao wameanza kupata huduma ya maji safi katika maeneo yao.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi blog.
WANANCHI zaidi ya 265 wa mtaa wa Upendo, Mbezi Salasala wilayani Kinondoni wamelishukuru Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), kwa kuwafikishia huduma ya Majisafi waliyoipatia shida kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.
Akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja wa serikali za mitaa na DAWASCO, Mjumbe wa mtaa wa Upendo Bw. Robert Massawe amepongeza juhudi zilizofanywa na Dawasco za kuwapatia huduma ya Maji wananchi wa eneo lake na kwamba juhudi hizo zinaendana na kauli ya serikali ya awamu ya tano inayosema hapa kazi tu.
Akieleza historia fupi ya eneo hilo Bw. Massawe alisema tangu watu waanze kuhamia eneo hilo huduma ya Maji ilikuwa ni ya kununua kutoka mtaa mwingine wa mbali ambao ulikuwa umefikiwa na huduma hiyo ya Maji.
RC Simiyu apiga mkwara mzito
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthon Mtaka
akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mwamgoba wilayani Busega (hawapo pichani)
kabla ya zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru
kaya maskini TASAF III kijijini hapo, Wilayani Busega Mkoani humo.
Na Stella Kalinga (Ofisi ya Mkoa wa Simiyu)
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amewataka viongozi wa kata na vijiji kuwabaini wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya TASAF III(PSSN) wanaojihusisha na ulevi na kuwaondoa katika orodha ya wanufaika wa mpango huo.
Mtaka ametoa agizo hilo wakati alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Mwamgoba wilayani Busega katika zoezi la uhawilishaji fedha za TASAF III PSSN, ambapo jumla ya shilingi 2,976,000 zimegawiwa kwa wanufaika 82 kijijini hapo.
Mtaka amesema lengo la mpango wa TASAF III ni kuwatoa watanzania katika hali ya umaskini kwa kuwapa ruzuku itakayowasadia kupata huduma muhimu ikiwa ni pamoja huduma za afya, kuwasaidia watoto wao waweze kwenda shule lakini baadhi ya wanufaika wamekuwa wakitumia fedha hizo kulewa badala ya kuanzisha miradi midogo midogo kama ufugaji wa kuku, mbuzi na kondoo pamoja na kilimo ili miradi hiyo iwasaidie kuwaongezea kipato.
STAMICO yatangaza neema kwa wachimbaji wa madini Tanzania
Katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wananufaika na kazi zao na kuepuka kuondolewa na wachimbaji wakubwa wameshauriwa kuchukua leseni ndogo za awali za uchimbaji.
Kaimu Mkurugenzi wa utafiti na Uchimbaji wa Shirika la Madini (STAMICO) Alex Rutagwelela (Katikati) akiongea na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa maonyesho ya Nane nane Viwanya vya Ngongo - Lindi.
Wito huo kwa wachimbaji umetolewa na kaimu mkurugenzi wa utafiti na uchimbaji wa shirika la madini (STAMICO) Alex Rutagwelela alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya ngongo Manispaa ya Lindi yanapofanyika maonyesho ya nane nane kitaifa.
Rutagwelela alisema wachimbaji wadogo wanatakiwa kuwa na leseni za awali zitakazowafanya wawe na haki kwenye maeneo wanayochimba. hivyo kuwa na uhakika wa kuto ondolewa bila taratibu na wachimbaji wakubwa kwenye maeneo wanayochimba.
Wananchi wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Maafisa wa STAMICO walipotembelea Banda lao katika Maonyesho ya Nane nane yanayoendelea Mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo.
Aliwahakikishia wanahabari na wananchi shirika hilo linania ya kuwainua wachimbaji wadogo kwa kufanyia tathimini maeneo wanayochimba ili waweze kujua kiasi cha madini na mashapo yaliyopo katika maeneo hayo.
Alisema wachimbaji wanaweza kupata fursa ya mafunzo ili waweze kupata ujuzi wa kuyafahamu mambo ya kijiolojia, vilevile watakuwa na uwezo wa kupata mikopo.
Hata hivyo alitahadharisha kwamba wanaweza kunufaika na fursa hizo ni wachimbaji wenye leseni. "Wachimbaji wenye leseni nilazima wainuliwe, wengi wao hawana mitaji wanachimba kipindi cha masika kwenye makorongo na kiasi wanachopata ni kidogo sana, kwamfano wilaya ya Ruangwa na mkoa huu unamadini ya aina nyingi na mengi wakiwezeshwa watanufaika," alisema Rutagwelela.
Akibainisha wachimbaji wadogo wanachimba kwa kubahatisha, hivyo shirika hilo lipotayari kuwasaidia kufanya tathimini na kuwaonesha kiasi cha mashapo yaliyopo katika maeneo wanayochimba.
Huku akitoa wito wawe tayari kwa uchangiaji kiasi kidogo cha fedha ambacho ni rafiki kwa wachimbaji wadogo kwa ajili ya gharama ya uendeshaji mitambo wakati wa kuchoronga, ikiwamo mafuta.
Akiongeza kusema STAMICO kwa niaba ya serikali imejipanga kuwasaidia kufikia malengo yao ya kiuchumi na kimaendeleo.

Bayport yakabidhi msaada wa jenereta Halmashauri ya Bumbuli
Na Mwandishi Wetu, Bumbuli
KUTOKANA na kukosa umeme katika ofisi za Halmashauri ya
Bumbuli, Taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, imemkabidhi jenereta
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi na
kufanikisha maendeleo kwa wakazi na wananchi wa Bumbuli, mkoani Tanga.
Meneja wa Bayport Financial Services, Kanda ya Kaskazini, Emmanuel Nzutu, kulia, akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bumbuli, Peter Nyalali kushoto baada ya kumkabidhi msaada wa jenereta kutoka kwenye taasisi yao ya Bayport kwa ajili ya ofisi ya Halmashauri ya Bumbuli ili iweze kujiendesha vizuri kutokana na ukosefu wa umeme kwenye majengo yao ya ofisi. Nyuma ya Nzutu ni Meneja wa Bayport wilaya ya Lushoto Consolata Thomas, akifuatiwa na Afisa Utumishi wa Bumbuli, Fatma Mrope. Picha na Mpiga picha wetu Bumbuli.Makabidhiano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki iliyopita yakiongozwa na Meneja wa Bayport Kanda ya Kaskazini, Emmanuel Nzutu, Meneja wa Bayport, wilayani Lushoto mkoani Tanga, Consolata Thomas, Mkurugenzi Mtendaji Bumbuli Peter Nyalali, Afisa Utumishi wa Bumbuli Fatma Mrope na baadhi ya watumishi wengine wa halmashauri hiyo.
Meneja wa Bayport Financial Services, Kanda ya Kaskazini, Emmanuel Nzutu, kulia, akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bumbuli, Peter Nyalali kushoto baada ya kumkabidhi msaada wa jenereta kutoka kwenye taasisi yao ya Bayport kwa ajili ya ofisi ya Halmashauri ya Bumbuli ili iweze kujiendesha vizuri kutokana na ukosefu wa umeme kwenye majengo yao ya ofisi. Nyuma ya Nzutu ni Meneja wa Bayport wilaya ya Lushoto Consolata Thomas, akifuatiwa na Afisa Utumishi wa Bumbuli, Fatma Mrope. Picha na Mpiga picha wetu Bumbuli.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Meneja wa Bayport Kanda ya Kusini, Nzutu, alisema kwamba taasisi yao imeona ikabidhi msaada wa jenereta kwa mkurugenzi wa Bumbuli ili watumishi kwenye ofisi hiyo watoe huduma bora na kwa wakati ili kuharakisha maendeleo katika serikali ya Hapa Kazi Tu, inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr John Pombe Magufuli.
“Bayport ni taasisi inayotoa huduma za mikopo huku tukifanya kazi kwa karibu na watumishi wengi nchini Tanzania, hivyo baada ya kuona ofisi za Halmashauri Bumbuli hazina umeme na wafanyakazi wanapata tabu, tukaona tuje kuwakomboa kwa kuwapa jenereta.
Sunday, August 07, 2016
Mshindi wa Airtel Trace Music azungumza na vijana Mwanza
Star wa Airtel Trace Music 2015, Mayunga Andrew Nalimi-MAYUNGA, akizungumza na #BMG kuhusiana na project yake ambayo anaifanya na star M-Rap.
Na George Binagi-GB Pazzo
Project inaitwa Across Lovers and Friend Music Tour ambayo Mayunga anaitumia kukutana na mashabiki zake na kuwapa burudani ikizingatiwa tangu atoke Marekani hakuwahi kufanya tour kama hiyo kwa ajili ya mashabiki zake.
Mayunga amesema Project hiyo imeanzia Mwanza na itaendelea katika mikoa mingine na hata nje ya nchi kama vile Kenya, Uganda, Malawi na Afrika Kusini.
Usiku huu anapiga show Jembe Beach Jijini Mwanza.
LHRC yampokea kwa shangwe mwanaharakati akitokea Marekani
Geline Fuko (kushoto) akipokea maua kutoka kwa wafanyakazi wenzake wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),ikiwa ni ishara ya kumpongeza baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jana, akitokea Marekani alikokuwa akihudhuria mafunzo ya vijana wa kiafrika yaliyoandaliwa na
Raisi Obama.
Na Dotto Mwaibale, Dar es Salam
SHANGWE ilitawala wakati mtanzania Geline Fuko alipo wasili Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) majira ya saa nne usiku jana Agosti 5, 2016 akitokea nchini Marekani alikohudhuria mafunzo ya viongozi vijana kutoka Bara la Afrika.
Wafanyakaziwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ambao ni wafanyakazi wenzake wa Geline, familia ya Geline, ndugu na marafiki walitoa mapokezi ya kishujaa wa wanaharakati huyo aliyetajwa kuwa mfano wa kuigwa na Rais Obama.
Akizungumza na wanahabari, Geline alisema amefarijika na hakutarajia kama wazo lake la kuanzishwa kwa Kanzidata ya Katiba litakuwa wazo kubwa ambalolitakubalika mpaka na Rais Obama.
Hata hivyo Geline alisema amefurahishwa na program hiyo ya Mandela Washington Fellowship kwani imewawezesha washiri kikujifunza mambo mengi na kupata uono mpana zaidi wakufanya mambo.
Wednesday, August 03, 2016
Mkuu wa Wilaya Ilala akabidhiwa msaada wa madawati
Video ya MH DC Ilala
Muwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania,Gou Haodong akimkabidhi moja ya dawati kati ya 100 yaliyotolewa na Wafanyabiashara wa Karikoo wenye asili ya China ,kwa Mkuu wa Wa Wilaya ya Ilala,Mh Sophia Mjema mapema leo jijini Dar.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mh Sophia Mjema akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa madawati 200 kutoka kwa Wafanyabiashara wa Kariakoo wenye asili ya China leo jijini Dar,kwa ajili ya shule ya msingi Maghorofani iliyopo Gongolamboto,jijini Dar Es Salaam.Wafanyabiashara hao waliahidi kumkabidhi Mh.DC Mjema Madawati 200 lakini leo wamekabidhi nusu ya madawati hayo (100),huku mengine yakiendelea kutengenezwa.Shule hiyo ya Maghorofani ilikuwa na uhitaji wa madawati 525, yakapatikana madawati 250 na kupungukiwa madawati 275.
Mkuu wa Mkoa Singida azindua maonyesho ya Nane Nane Kanda ya Kati Dodoma
Na Mathias Canal, Dodoma
UFUNGUZI wa siku ya wakulima Nane nane Kanda ya kati Dodoma mwaka 2016 umefanyika leo katika Uwanja wa Maonyesho ya kilimo Nzuguni Mkoani Dodoma huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni "Kilimo, Ufugaji na Uvuvi ni nguzo ya maendeleo, Kijana shiriki kikamilifu (Hapa Kazi Tu).
Mkuu wa Mkoa wa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe (Kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Nane Nane katika uwanja wa maonyesho ya kilimo Nzuguni Mkoani Dodoma.
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya za Dodoma na Singida wakiongozwa na Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Singida Mathew Mtigumwe wakikagua eneo la maonyesho ya bwawa la samaki lenye samaki aina ya perege, kambare na kamongo liloandaliwa na Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
Maonyesho haya yanahusisha shughuli za wakulima, wafugaji wa mifugo, wafugaji wa nyuki, wavuvi, wanamazingira, wasindikaji wa bidhaa za mazao ya kilimo na mifugo, wizara taasisi/makampuni ya umma, makampuni binafsi, mabenki, taasisi za umma na za binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Akizungumza katika ufunguzi huo Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe alisema kuwa sekta ya kilimo bado ni mhimili wa uchumi wa Tanzania kwa sababu inaajiri zaidi ya asilimia takribani 80 ya watanzania na kwa kuzingatia malengo ya maendeleo ya Taifa ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati unaotegemea viwanda hivyo kilimo kikiboreshwa viwanda vitapata malighafi ya uhakika na kuimarisha masoko kwa wakulima hivyo kuwepo na ajira ya kuaminika kwa vijana na watanzania kwa ujumla.
RC Mtigumwe alisema kuwa wastani wa ukuaji wa sekta ya kilimo unabadilika mwaka hadi mwaka kutokana na kilimo kwa kiwango kikubwa kutegemea mvua ambazo zimekuwa zikinyesha kwa viwango na mtawanyiko unaotofautiana kila mwaka ambapo kwa mwaka 2010 sekta ya kilimo ilikuwa kwa asilimia 4 ikilinganishwa na asilimia 6.5 ya mwaka 2015.

TV 1 kurusha matangazo ya mpira wa miguu Uingereza
Mkuu wa TV 1, Joseph Sayi (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu, Kituo cha Televisheni cha TV1 Tanzania kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ya Ligi Kuu soka ya Uingereza EPL yatakayoanza Agosti 13 mwaka huu. Kulia ni Meneja Masoko wa TV 1, Gillian Rugumamu na Meneja Masoko Startimes, kushoto ni Felix Awino.
Meneja Masoko wa TV 1, Gillian Rugumamu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu,Kituo cha Televisheni cha TV1 Tanzania kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo ambayo yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti 13 mwaka huu. Kushoto ni Mkuu wa TV 1, Joseph Sayi na kulia ni Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey Abdallah.
Jamii yaaswa kuwaunga mkono mabinti wanaofanya urembo
warembo wanaoshiriki shindano la miss kanda ya kaskazini kutoka katika
mikoa ya Arusha,Manyara,Tanga na Kilimanjaro wakiwa nje ya hotel ya
Clous view sehemu ambayo wanafanyia mazoezi kwa ajili ya shindano hilo
linalofanyika july 6 katika viwanja vya ukumbi wa Triple A fm
warembo hao wakiwa katika pozi .
Na Woinde Shizza, Arusha
Na Woinde Shizza, Arusha
Jamii imetakiwa kuwapa ushirikiano wa kutosha wasichana wanaoshiriki mashindano ya urembo kwani mashindano hayo ni kazi kama vile kazi zingine.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la kumsaka mrembo wa kanda ya kaskazini (Miss Kanda ya kaskazini )wakati walipokuwa wakiongea kwa nyakati tofauti na mwanandisi wa habari hizi ndani ya hotel ambayo warembo hao wameweka kambi kwa ajii ya shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mapema jumamosi July 6 katika ukumbi wa Triple A uliopo jijini Arusha.
UKUTA ya Chadema yapigwa marufuku mkoani Mbeya
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametangaza kupiga marufuku maandamano YA operesheni Ukuta yanayokusudiwa kufanywa tarehe 1 septemba badala yake waandaaji kujikita zaidi kubuni shughuli zenye tija kwa ajili ya wananchi wa mkoa wa Mbeya.
Mkuu wa Mkoa Mbeya, Mheshimiwa Amos Makalla, pichani akizungumza jambo katika kikao cha ulinzi na usalama wa mkoa wa Mbeya.
Amewaonya watakaokaidi tamko hilo watadhibitiwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Tamko hilo amenitoa leo kwenye kikao cha kazi kilichohusisha vyombo vya ulinzi na usalama, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na watendaji wa halmashauri zote za Mkoa wa mbeya. Amewashukuru wananchi wa mkoa wa Mbeya kwa namna walivyoonyesha utulivu na kutoshabikia operesheni Ukuta.
Amewataka wabunge na madiwani kufanya mikutano mingi kadri wanavyoweza katika maeneo yao kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi kero mbalimbali za wanachi na kilichokatazwa ni mikutano ya kashfa na kualika viongozi nje YA majimbo yao na mkoa.
Kuhusu uhakiki wa madawati ametoa siku 7 kwa wakuu wa wilaya kwa kushirikiana na waratibu elimu kata , viongoji vijiji, madiwani, maafisa elimu na wakurugenzi kuhakiki usambazaji wa madawati unaendana na taarifa za utengenezaji na upungufu uliobainishwa awali na mapokezi YA madawati hayo yathibitishwe na walimu wakuu wa shule.
Sambamba na hilo amewataka wahakiki pia wanafunzi waliopo mashuleni ili kudhibiti wanafunzi hewa kwa lengo la kupatiwa fedha zaidi katika zoezi la elimu bure. Amezitaka halmashauri zote kukamilisha ujenzi wa matundu ya vyoo na kuziwekea uzio shule zote ifikapo Desemba mwaka huu. Mkoa katika vipaumbele vyake ni kuboresha ukusanyaji mapato na ujenzi wa miundombinu ya Shule ikiwemo madarasa, vyoo, maabara, mabweni na nyumba za walimu.