Pages

Pages

Wednesday, August 03, 2016

UKUTA ya Chadema yapigwa marufuku mkoani Mbeya

Na Mwandishi Wetu, Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametangaza kupiga marufuku maandamano YA operesheni Ukuta yanayokusudiwa kufanywa tarehe 1 septemba badala yake waandaaji kujikita zaidi kubuni shughuli zenye tija kwa ajili ya wananchi wa mkoa wa Mbeya. 
Mkuu wa Mkoa Mbeya, Mheshimiwa Amos Makalla, pichani akizungumza jambo katika kikao cha ulinzi na usalama wa mkoa wa Mbeya.
Amewaonya watakaokaidi tamko hilo watadhibitiwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Tamko hilo amenitoa leo kwenye kikao cha kazi kilichohusisha vyombo vya ulinzi na usalama, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na watendaji wa halmashauri zote za Mkoa wa mbeya. Amewashukuru wananchi wa mkoa wa Mbeya kwa namna walivyoonyesha utulivu na kutoshabikia operesheni Ukuta.

Amewataka wabunge na madiwani kufanya mikutano mingi kadri wanavyoweza katika maeneo yao kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi kero mbalimbali za wanachi na kilichokatazwa ni mikutano ya kashfa na kualika viongozi nje YA majimbo yao na mkoa.

Kuhusu uhakiki wa madawati ametoa siku 7 kwa wakuu wa wilaya kwa kushirikiana na waratibu elimu kata , viongoji vijiji, madiwani, maafisa elimu na wakurugenzi kuhakiki usambazaji wa madawati unaendana na taarifa za utengenezaji na upungufu uliobainishwa awali na mapokezi YA madawati hayo yathibitishwe na walimu wakuu wa shule.

Sambamba na hilo amewataka wahakiki pia wanafunzi waliopo mashuleni ili kudhibiti wanafunzi hewa kwa lengo la kupatiwa fedha zaidi katika zoezi la elimu bure. Amezitaka halmashauri zote kukamilisha ujenzi wa matundu ya vyoo na kuziwekea uzio shule zote ifikapo Desemba mwaka huu. Mkoa katika vipaumbele vyake ni kuboresha ukusanyaji mapato na ujenzi wa miundombinu ya Shule ikiwemo madarasa, vyoo, maabara, mabweni na nyumba za walimu.

No comments:

Post a Comment