Pages

Pages

Sunday, June 26, 2016

Rais wa VoWET azindua umoja wa wanafunzi wa biashara

Rais wa VoWET na Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA Construction  Limited Bi. Maida Waziri akiongea na wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu  TIA wakati wa uzunduzi rasmi wa umoja wa wanafunzi wa Biashara (BAA), ambapo aliwahimiza elimu wanayoipata wasiitumie kwenda kuombea kazi tuu lakini pia waitumie kwa ajili ya kufanya ujasiliamali kwa kujiajili wao wenyewe.
Rais wa VoWET na Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA Construction  Limited Bi. Maida Waziri akikata keki ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa umoja huo.
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa  BAA Gwamaka Andrew (Kushoto) akimmkabidhi Cheti cha Shukurani Mgeni rasmi Bi. Maida Waziri (Kulia)

Wakuu wa wilaya wapya watangazwa, mtangazaji wa ITV Godwin Gondwe apewa Handeni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli, amefanya uteuzi wa wakuu wa wilaya, huku mwandishi na mtangazaji wa kituo cha ITV, Godwin Gonde, akitangazwa kupewa nafasi ya ukuu wa wilaya ya Handeni, akichukua nafasi ya DC Husna Rajab aliyeondolewa kwenye nafasi hiyo.

UTEUZI WA WA WAKUU WA WILAYA NCHINI.
ARUSHA
Arusha - Mrisho Mashaka Gambo
Arumeru - Alexander Pastory Mnyeti
Ngorongoro - Rashid Mfaume Taka
Longido - Daniel Geofrey Chongolo
Monduli - Idd Hassan Kimanta
Karatu - Therezia Jonathan Mahongo
DAR ES SALAAM
Kinondoni - Ally Hapi
Ilala - Sophia Mjema
Temeke - Felix Jackson Lyaviva
Kigamboni - Hashim Shaibu Mgandilwa
Ubungo - Hamphrey Polepole
DODOMA
Chamwino - Vumilia Justine Nyamoga
Dodoma - Christina Solomon Mndeme
Chemba - Simon Ezekiel Odunga
Kondoa - Sezeria Veneranda Makutta
Bahi - Elizabeth Simon
Mpwapwa - Jabir Mussa Shekimweli
Kongwa - John Ernest Palingo
GEITA
Bukombe - Josephat Maganga
Mbogwe - Matha John Mkupasi
Nyang'wale - Hamim Buzohera Gwiyama
Geita - Herman C. Kipufi
Chato - Shaaban Athuman Ntarambe
IRINGA
Mufindi - Jamhuri David William
Kilolo - Asia Juma Abdallah
Iringa - Richard Kasesela
KAGERA
Biharamulo - Saada Abraham Mallunde
Karagwe - Geofrey Muheluka Ayoub
Muleba - Richard Henry Ruyango
Kyerwa - Col. Shaban Ilangu Lissu
Bukoba - Deodatus Lucas Kinawilo
Ngara - Lt. Col. Michael M. Mtenjele
Missenyi - Lt. Col Denis F. Mwila

Tuesday, June 14, 2016

PPF wakabidhi vyeti vya wafanyakazi bora

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhani  Khijjah, akizungumza na baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko huo wakati wa zoezi la kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha Mikutano Dar es Salaam, (DCC).  Tukio hilo lilifanyika wakati wa Kikao cha Baraza la wafanyakazi. Picha na Mafoto Blog

Akizungumza baada ya kukabidhi Vyeti hivyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Ndugu Khijjah, aliwapongeza Wafanyakazi bora wa 2015/16 wa Mfuko huo kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini na kuwataka Wafanyakazi wote wa PPF kufanya kazi kwa bidii bila kurudi nyuma  ili kuendelea kutimiza malengo.
Katika Kikao hicho jumla ya Wafanyakazi 22,  kutoka Kurugenzi na Idara mbalimbali walikabidhiwa vyeti vya Wafanyakazi Bora na Mwenyekiti huyo.

Naibu Kadhi Mkuu Zanzibar ahudhuria mashindano ya kusoma quraan

 
Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Mashindano ya Kitaifa ya Kuhifadhi Qura-an Zanzibar yalioandaliwa na Jumuiya ya Kihifadhi Quran Zanzibar Naibu Kadhi Mkuu Zanzibar Shekh.Hassan Othma Ngwali(katikati) Amiri wa Jumuiya ya  Kuhifadhi Quran Zanzibar Mwalim Suleiman Omar Naimi Amiri Kuhifadhisha Quran Zanzibar Shekh. Mohammed Alawi Ally, wakifuatilia mashindano hayo yaliowashirikisha Wanafunzi wa Vyuo vya Quran Zanzibar,Tanga Pwani na Morogoro. 

Thursday, June 09, 2016

RC Mwanza akabidhi visiwa kwa Maliasili

Na Atley Kuni- RS Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, ameiagiza taasisi ya taaluma ya wanyamapori Pasiansi kuanza kutumia visiwa na majabali makubwa yaliopo mkoani humo kwaajili ya mazoezi ili kuweza kusaidia kupambambana na uhalifu ulioanza kujitokeza katika siku za karibuni katika mkoa huo.
Akizungumza katika uzinduzi wa maonesho ya sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho nchini Tanzania, Mongella amesema badala ya wakurufunzi hao kwenda kufanya mazoezi kwenye maeneo ya nje ya mkoa ni vema kuanzia sasa mkaanza kutumia visiwa vyetu,
“Ndani ya ziwa viktoria, hasa huko visiwani kuna watu wanafanya uvuvi haramu sasa ni vema wakati wa mazoezi mkawa mnafanyia kwenye maeneo hao ambayo yamekithiri kwa uvuvi usio na tija”, alisema Mongella na kuongeza, “lakini sio kukomesha tuu, uvuvi haramu bali pia itachagiza kwenye suala zima la utunzaji wa mazingira na maliasili”
Amesema kuwa, endapo taasisi hiyo ikitumia sehemu ya mafunzo kwa vitendo, kama mkoa utakuwa hauna haja yakufunga shughuli za uvuvi kwa msimu na badala yake itasaidia kwenye uzazi salama wa samaki na viumbe wengine wa majini.

Watumishi hewa 170 wabainika mkoani Mbeya na kuleta hasara ya Sh 773,882,066

Na Mwandishi Wetu, Mbeya
Serikali Mkoa wa Mbeya imebaini watumishi hewa 170 kutokana na uhakiki ulifanywana timu ya vyombo vya dola iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa mbeya tarehe 20 April mwaka huu na idadi ya watumishi hewa imesababisha hasara ya she 773,882,066.

Hayo amesema leo na Mkuu wa mkoa wa Mbeya alipokutana na waandishi wa habari kutangaza matokeo ya timu akiyoiunda kuhakiki watumishi hewa. Pamoja na hasara hiyo watumishi hewa 58 kati ya 170 wamekopa mikopo katika benki jumla ya shilingi 481,574,351

Serikali pamoja na kufanya uhakiki iliwataka watuhumiwa kurejesha fedha zote zi kikubwa katika akaunti na sh 65,058,542. Mkuu wa mkoa amewaagiza wakurugenzi kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuwasaka popote walipo watumishi hewa na kuwachukulia hatua za kisheria.


Aidha amewaagiza wakurugenzi, maafisa utumishi na maafisa wa mfumo kuwajibika kwa kuendelea kulipa watumishi hewa. Kuanzia sasa kila afisa utumishi atawajibika kuwaondoa watumishi watoro pale wanapibainika na amewataka wakurugenzi kuwa na mpango endelevu wa kudhibiti watumishi hewa

Kanisa la Sinza Christian Center latupiwa vyombo vyake nje

Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa.
HALI ya sintofahamu imeibuka baada ya Kanisa la Sinza Christian Center lenye maskani yake Sinza, jijini Dar es Salaam kutupiwa vyombo vyake nje kwa madai ya kudaiwa deni la pango la jengo hilo jumla ya Sh Milioni 100.

Mmiliki wa jengo hilo anatajwa kuwa ni Prosper Rwendera, huku amri ya kutoa vyombo nje vya kanisa hilo ikitolewa na mahakama kwa madai kuwa upangaji huo ulikuwa na utata.

Alipotafutwa msemaji wa Kanisa ambaye ni Askofu anayedaiwa kuvamia jengo hilo, hakupatikana kuzungumzia sakata hilo na hata waumini wa kanisa hilo walipotafutwa walikataa kwa madai hawana mamlaka ya kuzungumzia lolote kuhusiana na sakata hilo.
Hili ni eneo la Kanisa Hilo.

Wateja wa viwanja vya Bayport waendelea kupewa hati zao

Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, katikati akizungumza baada ya kumpa hati yake mteja wao wa viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, Ibrahim D Mahinya. Kulia ni Afisa Sheria wa Bayport, Mrisho Mohamed.

Na Rahim Kambi, Dar es Salaam
TAASISI ya Kifedha ya Bayport inayojihusisha na mikopo imeendelea kugawa hati za viwanja kwa wateja wao walionunua viwanja katika mradi wao uliopo Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, uliozinduliwa rasmi mwezi Mei mwaka jana.


Wateja waliokabidhiwa hati zao ni pamoja na Ibrahim D Mahinya na Desdery Selestine Mkenda ambao wote kwa pamoja walikuwa miongoni mwa wateja waliojiunga na huduma hiyo ya mikopo ya viwanja vya Bayport.
Ibrahim Mahinya kushoto akizungumza jambo baada ya kukabidhiwa hati ya kiwanja cha Vikuruti, kutoka Bayport Financial Services, jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Mwenye miwani ni Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme na Mrisho Mohamed, Afisa Sheria wa Taasisi hiyo inayohusisha na mikopo ya fedha na bidhaa vikiwamo viwanja.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika makabidhiano hayo, Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, alisema kusudio lao ni kugawa hati kwa wateja wao mapema iwezekanavyo ili kujitofautisha na wadau wengine wanaojihusisha na mambo ya uuzaji wa ardhi kwa njia mbalimbali.

Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme katikati akimkabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti mteja wao Desdery Selestine Mkenda. Kulia ni Mrisho Mohamed, Afisa Sheria wa Taasisi hiyo inayohusisha na mikopo ya fedha na bidhaa vikiwamo viwanja.

Alisema kwamba hati zinazotoka kwa mwaka huu ni zile zinazohusu wateja walionunua viwanja hivyo katika mradi wa Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, mradi uliopokewa vizuri na Watanzania, jambo lililochangia Bayport kupanua wigo huo kwa kuanzisha miradi mingine ya Bagamoyo, Kigamboni, Chalinze, Kibaha na Kilwa.

Tuesday, June 07, 2016

Jeshi la Polisi Tanzania lapiga marufuku mikutano ya kisiasa na maandamano

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu zangu waandishi wa habari,
Katika siku za hivi karibuni, Jeshi la Polisi nchini, limepokea taarifa kutoka kwa baadhi ya vyama vya siasa wakitaka kufanya mikutano na maandamano . hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia vyanzo vyake vya mbalimbali vya habari limebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi (Civil disorder).
Aidha vyama vingine vya siasa vimeonyesha dhamira ya kupinga kile ambacho kitasemwa na wapinzani wao.
Vyanzo hivyo vya habari vimebainisha kwamba upo uwezekano mkubwa wa kutokea vurugu baina ya makundi mawili ya kisiasa.
Kwa hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linapiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kuanzia tarehe 07/06/2016 hadi hapo hali ya usalama itakapotengemaa.
Jeshi la Polisi linawataka wanasiasa kuacha mara moja kuwashinikiza wananchi kutotii sheria za nchi.
Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote au chama chochote cha siasa kitakachokaidi agizo hili.
Aidha Jeshi la Polisi linawataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wenye lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi hii na badala yake linawasihi waendelee kushirikiana katika kujenga umoja wa nchi hii.
Asanteni sana kwa kunisikiliza .
Imetolewa na:-
Nsato M. Mssanzya – CP
Kamishina wa Polisi Operesheni na Mafunzo
Makao Makuu ya Polisi

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya awakalia kooni kampuni ya SICO

Na Mwandishi Wetu, Mbeya
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla, katikati mwenye miwani, leo amekagua barabara zenye urefu wa kilometa 23 zilizojengwa miaka 2 iliyopita katika mitaa ya jiji la Mbeya na kubaini baadhi ya Barabara zilijengwa chini ya kiwango na zingine zi kuharibika na malori ya mizigo yenye uzito mkubwa kuliko uwezo wa barabara. Aidha Baadhi ya barabara kukosa mifereji ya kupitisha Maji na kusababisha uharibifu kwa wanafunzi wa Chuo kikuu cha TEKU
Kufuatia taarifa za wananchi juu ya Uwepo wa mashimo na kuanza kubomoka kwa baadhi ya barabara hizo imemlazimu Mkuu wa mkoa kufanya ziara kukagua barabara hizo na kuagiza mkandarasi SICO Ltd kurekebisha kasoro zote zilizojitokeza na kuongeza tanaka la lami kwa barabara soko la Kebwe yanakoingia magari makubwa na mkandarasi amekubali na kazi hiyo imeanza mara moja.

Pia ameagiza uongozi wa jiji kushughulikia Kero ya mifereji na kwakuwa Tamisemi wametoa fedha mkandarasi wa kujenga na kupanua mifereji ataanza kazi tarehe 1 julai mwaka huu
Anewataka madiwani wa halmashauri zote na jiji la mbeya kuwa makini na wafuatilisji wa miradi kwani inasikitisha kuwaona barabara iliyokabidhiwa miaka 2 iliyopita tena yenye thamani kubwa yavfedha bilioni 23 katika kipindi kifupi barabara zinakuwa na mashimo lakini hawakuchukua hatua zozote na wananchi wananungungunika
Hivyo amewataka viongozi na watalaam kutanguliza uzalendo na wahakikishe miradi inatekelezwa kwa viwango vya juu