Pages

Pages

Sunday, June 26, 2016

Rais wa VoWET azindua umoja wa wanafunzi wa biashara

Rais wa VoWET na Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA Construction  Limited Bi. Maida Waziri akiongea na wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu  TIA wakati wa uzunduzi rasmi wa umoja wa wanafunzi wa Biashara (BAA), ambapo aliwahimiza elimu wanayoipata wasiitumie kwenda kuombea kazi tuu lakini pia waitumie kwa ajili ya kufanya ujasiliamali kwa kujiajili wao wenyewe.
Rais wa VoWET na Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA Construction  Limited Bi. Maida Waziri akikata keki ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa umoja huo.
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa  BAA Gwamaka Andrew (Kushoto) akimmkabidhi Cheti cha Shukurani Mgeni rasmi Bi. Maida Waziri (Kulia)
Afisa Taaluma wa Chuo cha uhasibu TIA na Kaimu Mkurugenzi wa Chuo hicho Bw. Mugisha Kamala akitoa neno la utangulizi na shukurani kwa watu wote waliohudhuria katika uzinduzi huo.
Aliyekuwa Afisa Mipango wa BAA Alex Mujwahuzi akitambulisha baadhi ya Viongozi waliokuwepo katika uzinduzi huo
Afisa Mipango msaidizi mstaafu wa BAA Bi. Grace Samagoda akisoma risala kwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo 
Aliyekuwa mwenyekiti wa BAA ambaye amemaliza muda wake Bw. Elisha Benard akitoa historia ya umoja huo
Mwenyekiti mpya wa BAA Bw. William Msemo akitoa neno la shukurani kwa kuchaguliwa pamoja na kuwaomba ushirikiano wanafunzi wenzake katika kipindi chote atakachokuwa madarakani.
Afisa Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Delphin Richard akiwahimiza wanafunzi wa chuo cha TIA kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa Hiari (PSS) ambapo pamoja na yote ataweza kupata Fao la Elimu.
Mratibu Mkuu wa Shughuli za kampuni ya Tone Multimedia Chande Abdallah akiwatambulisha wanafunzi wa chuo cha TIA blog ya wanachuo ya Matukio na wanavyuo ambapo mwanachuo yeyote atapata nafasi ya kupata matukio na Taarifa mbalimbali za wanavyuo nchini Tanzania.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Uzinduzi rasmi wa umoja wa wanafunzi wa Biashara BAA Gwamaka Andrew akitoa neno la Shukurani kwa kufanikisha vema shughuli hiyo.
Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu (TIA) wakiwa katika uzinduzi wa BAA
 Mgeni Rasmi akipata picha ya pamoja na Baadhi ya Viongozi wa BBA waliomaliza muda na wale wa sasa
Picha zote na Fredy Njeje 


No comments:

Post a Comment