Pages

Pages

Sunday, May 15, 2016

Zahir Zoro alitikisa jiji la Mwanza

Mwanamuziki wa siku nyingi nchini kwenye muziki wa dansi na rumba, Zahir Ally Zoro (pichani) usiku wa kuamkia leo (jumamosi mei 14,2014) amewaburudisha wakazi wa Jiji la Mwanza baada ya kufanya show kali katika Ukumbi wa Kilimanjaro Hotel, Nyegezi.

Ilikuwa ni show yake ya kwanza kwa mwaka huu 2016 ambapo wapenzi wa muziki wa dansi na rumba walivutiwa na burudani iliyotolewa na Zoro hasa baada ya kuimba live wimbo uitwao "Beatrice" ambao ni wimbo uliofanya vizuri sana wakati anauachia akiwa na band yake ya Mass Media.

Burudani kutoka kwa Zahir Ally Zoro ikiendelea.
JJ Band kutoka Jijini Mwanza, pia walifanya show kali katika kumsindikiza Zahir Ally Zoro.
Ilikuwa Show Kali sana ikizingatiwa kwamba wakazi wa Jijini la Mwanza huwa wanaumiss muziki wa dansi/rumba.
Twiga Band kutoka Jijini Mwanza pia walimsindikiza Mzee Zahir Ally Zoro ambapo walifanya show nzuri na hivyo kuonyesha kwamba kwa siku za hivi karibuni Mwanza kutakuwa na band nzuri.
Zahir Ally Zoro (Kushoto) akiwa katika mahojiano baada ya show. Anasema alifarijika sana baada ya Wakazi wa Jiji la Mwanza kufurahia burudani yake jukwaani ambapo alisisitiza zaidi media za Mwanza kusupport muziki wa dansi ili kuurudisha kwenye chat.
Zahir Ally Zoro (Kushoto) akizungumza na Slyvester Joseph kutoka BMG na Afya Radio ya Jijini Mwanza.
Zahir Ally Zoro akiwa na bango la 102.5 Lake Fm Mwanza.
Mkurugenzi wa Kilimanjaro Hotel, Joseph Chuwa, akizungumzia show ya Zahir Ally Zoro ambapo anasema Mwanza huwa wanamiss muziki wa dansi hivyo atahakikisha mara kwa mara anawaletea wanamuziki hao ili kuwaburudisha wanamwanza na kuongeza kwamba pia leo jumapili kutakuwa na Family Bonanza ambapo JJ Band, Twiga Band pamoja na Zahir Ally Zoro watatoa burudani.
Slyvester Joseph kutoka BMG & Afya Radio (kushoto) akifanya mahojiano na Alphonce Tonny Kapela (kulia) kutoka Metro Fm Mwanza kuhusiana na muziki wa dansi pamoja na show ya Zahir Ally Zoro.

No comments:

Post a Comment