Pages

Pages

Thursday, October 22, 2015

Wateja wa Bayport sasa kukopeshwa simu za mikononi

Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, pichani akizungumza jambo katika moja ya shughuli za taasisi hiyo nchini.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SEKTA ya mawasiliano ni kati ya mambo muhimu na mazuri inayoweza kufanikisha kwa vitendo kukuza uchumi wa Taifa letu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kusimamia vyema sekta hiyo, uchumi wa Wwatanzania utakuwa kwa kasi.

Na katika mambo yaliyokuwa kwenye kundi hilo la mawasiliano, ni kuona Watanzania wanawasiliana kwa kumiliki simu imara ili waweze kuwasiliana katika mahitaji yao ya kimaisha, bila kusahau biashara na wajasiriamali.

Si lazima mtu aende mkoani Mbeya, Tanga, Arusha kufuata au kupeleka bidhaa zake bila kufanya uchunguzi swa soko, hususan kwa kuwasiliana na watu wanaoishi huko, au wale wanaoshirikiana katika majukumu yao ya kila siku.
Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo imezindua huduma yake mpya ya mikopo ya simu za mikononi kwa ajili ya kutoa fursa kwa Watanzania waweze kumiliki simu imara na za kisasa, yani smartphone ‘Jibayportphonishe’.

Katika huduma yao hiyo, Bayport wanashirikiana na Kampuni ya Cape View, ambapo mteja akikopa simu anapelekewa hadi eneo analohitaji simu hiyo ifike, jambo linalotafsiriwa kuwa ni mkombozi wa wateja wao na Watanzania kwa ujumla.

Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, anasema kwmbahuduma hiyo mpya itapatikana katika mikoa yote ya Tanzania Bara kwa kupitia matawi yao 80 nchi nzima.

Anasema simu hizo ni aina ya Huawei Ascend Y220, ambazo zinapatikana kwa Sh 140,000 tu, huku mteja akiweza kukopeshwa na yeye akilazimika kuilipia Sh 9000 tu kila mwezi katika kipindi cha miezi 24, sawa na miaka miwili tu.

“Hii ni huduma rahisi na muhimu kwa wateja wetu katika kundi la watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa na taasisi yetu, huku tukiamini kuwa kuanzishwa kwa huduma hii kutapanua uchumi wa nchi yetu.

“Mteja wetu anaweza kukopa simu kuanzia moja hadi simu tano na kuzitumia kadri anavyoona inafaa, hususan kwenye familia zao, ukizingatia kuwa wapo watu wanaoweka kidogo kidogo ili wanunuwe simu nzuri, hivyo hii ni nafasi yao,” Alisema Cheyo.

Cheyo anasema kwamba wapo wazazi wanaoishi mbali na watoto wao, hususan watoto wao wanaosoma mikoani katika vyuo mbalimbali, ambapo wamekuwa wakishindwa kuwasiliana kwa wakati, hivyo huu ni wakati mzuri kwao kuona watu wanaunganishwa kwa kupitia simu za mikopo ya Bayport kwa kushirikiana na kampuni ya Cape View.

Anasema kwamba kwa kupitia simu hizo, ulimwengu umekuwa rahisi kutokana na simu hizo ambazo zina huduma zote za internet kama vile whatssap, facebook, twitter, yahoo, gmail na mitandao mingine, huku kampuni ya Simu za Mikononi ya Vodacom Tanzania, ikitoa ofa ya vifurushi vya MB500 kwa miezi sita kila simu atakayopata mteja itaunganishwa moja kwa moja.

Meneja Masoko huyo na Mawasiliano wa Bayport anasema kwamba ni tumaini lao kwamba wateja wao wataiu nga mkono huduma hiyo mpya maana ipo kwa ajili yao, wakiamini kuwa kupata simu hizo ni sehemu ya kukuza uchumi wao.

“Huu ni wakati wa kuona nchi yetu inasonga mbele kwa kuhakikisha kwamba taasisi za kifedha kama yetu ya Bayport inabuni mambo yanayorahisisha maisha ya watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi zilizoidhinishwa, maana ndio jambo linaloweza kuifanya nchi yetu iwe na uchumi imara.

“Huu ni wakati wa wateja wetu kuhakikisha wanakopeshwa simu hizi na sisi Bayport na wenzetu Cape View tutawafikishia simu hizo hadi katika maeneo yao wanayopatikana, ikiwa ni njia inayoondoa usumbufu wote, kama wale wanaotoa gharama za nauli ili kufuata simu maeneo ya mbali, hivyo tunaamini huu ni wakati mzuri kwao kwa kuchangamkia simu hizi za Huawei ambazo kila simu itakuwa na waranti ya mwaka mmoja,” Alisema.

Kuanzishwa kwa huduma hiyo ya simu za mikopo, ni mwendelezo wa taasisi ya Bayport kubuni na kuendesha huduma mbalimbali zinazochangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa Watanzania. Mbali na kukopesha fedha, Bayport pia inatoa huduma ya mikopo ya viwanja katika mradi wa Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, huduma ya Bima ya Elimu kwa uwapendao, Bima ya Magari, mikopo ya bidhaa na nyinginezo.

Naye Mkurugenzi wa Cape View, Micka Mavoa, anasema kwamba simu hizo ni za kisasa za Huawei zinaokwenda kwa dhamira ya kurahisisha maisha ya Wwatanzania wote, wakiwamo watumishi wa qumma na wale wa kampuni zilizoidhinishwa.

“Hii ni zaidi ya Jibayportphonishe kwa sababu ni simu bora zenye viwango vyote vya kuwapatia maisha bora Watanzania watakaopenda kupata simu zetu kwa njia ya mkopo na wao wakiweza kulipa Sh 9000 tu kila mwezi.

“Ili mteja apate simu hiyo, anapaswa kuchukua fomu ya maombi katika ofisi ya Bayport iliyopo karibu yake , ambapo baada ya mkopo wake kuthibitishwa na kufanikiwa, atapelekewa simu yake popote alipokuwa,” Alisema.

Kwa mujibu wa Mavoa, wazo la kukopesha simu kwa wateja limekuja ili kuwafanya Watanzania wamiliki simu za kisasa bila kusubiria wawe na fedha nyingi, huku akisema maisha yatakuwa rahisi endapo Watanzania wataiunga mkono huduma hiyo ya aina yake.

Anasema mshahara wa mteja utafanya kazi nyingine za kimaendeleo kwa kutoa kiasi kidogo cha Sh 9000 tu kama sehemu ya makato ya mkopo huo wa simu utakaomuwezesha kuiweka Dunia katika kiganja chake.

Bayport ni Taasisi ya kifedha isiyo ya kibenki inayoongoza katita utowaji wa mikopo barani Afrika na Amerika ya Kusini, ikianzishwa mwaka 2001, na umiliki wake ukiwa nchini Mauritius, huku ikipatikana pia Botswana, Ghana, South Africa, Tanzania, Uganda, Zambia na sasa Columbia, ambapo hadi wakati huu Bayport imehudumia zaidi ya wateja 320,000 kupitia matawi yake 235 na zaidi ya wafanyakazi 2,500.

Nchini Tanzania, Bayport ilianzishwa mwaka 2006 na kwa kasi imekuwa taasisi inayo ongoza katika utoaji wa mikopo kwa watumishi wa serikali na wafanyakazi wa makampuni binafsi yaliyoidhinishwa, huku ikiwa na matawi 80 katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara, ambapo mteja anaweza kukopa pia kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz.

No comments:

Post a Comment