Pages

Pages

Thursday, October 22, 2015

Mke wa Dkt Shein achanja mbuga kumuombea kura mumewe visiwani Zanzibar

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwasili katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere Bububu kwa ajili ya kuzungumza na Viongozi wa Wanawake wa Wilaya ya Mfenesini Unguja Kichama kuwaombea Kura Wagombea Wote wa Chama cha Mapinduzi CCM.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Mfenesini Unguja Kichama akitowa salamu za Wilaya yake kwa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, kabla ya kuaza kwa mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Bububu.
Viongozi wa UWT Wilaya ya Mfenesini Unguja wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Bububu wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia na kuwaomba kura kuwapigia Wagombea wote wa CCM.
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Salama Aboud Talib akizungumza na kumkaribisha Mama Fatma Karume kuzungumza na Wanachama wa CCM kupitia UWT Wilaya ya Mfenesini Unguja. na kuwakumbusha siku ya kupiga kura kuitumia siku hiyo viziri kukipigia kura ya ndio Chama cha Mapinduzi. 
Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume amuwataka Wanawake kujitokeza kwa wingi kukipigia Kura Chama cha Mapinduzi ili kukipatia ushindi wa kishindo na kusisitiza wasipoteze kura zao wakati wao Mwanake alikuwa haruhusiwi kupiga kura. wakati wa ukoloni 
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif akizungumza na Wanawake wa Wilaya ya Mfenesini Unguja na kuwataka kutumia nafasi zao kutowa elimu kwa wananchi kuhamasika kujitokea kwa wingi kuipiga kura siku ya tarehe 25/10/2015.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Mama Asha Balozi akisisitiza jambo wakati wa mkutano na Wanawake wa Wilaya ya Mfenesini Unguja kuwahamasisha kujitokeza kwa wingi katika kupiga kura kwa Wagombea wa CCM. 
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania WEilaya ya Mfenesini Unguja wakati akiwa katika ziara yake kuwatwembelea Viongozi wa Wanawake Zanzibar kuwapigia kampeni Wagombea wa CCM kwa Wananchi kupitia Wanawake.
Viongozi wa jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania UWT wakimsikilza Mama Mwanamwema Shein, wakati akiwahutubia na kuwaombea kura Wagombea wa CCM.

 Mgombea Uwakilishi Jimbo la Bububu  Masoud Abdurahaman akiomba kura na kuwaombea kura Wagombea wote wa CCM na Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli. 
Mgombea Ubunge Jimbo la Mfenesini kwa tiketi ya CCM Kanali Mstaaf Masoud akiomba kura kwa Viongozi wa UWT waliohidhuria mkutano wa Mama Mwanamwema Shein, kuwaombea kura Wagombea Urais wa Zanzibar na Tanzania kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein na Dk John Pombe Magufuli.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Welezo Mhe Saada Mkuya, akiomba kura kwa Viongozi wa UWT wakati wa mkutano na Mama Mwanamwema Shein, uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Malimu Nyerere Bububu Zanzibar. 
Wanachama wa CCM Jumuiya ya UWT wakimshangilia Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein wakati akiwatambulisha Wagombea Ubunge na Uwakilishi wa Wilaya ya Mfenesini Unguja wakati wa mkutano wake uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Bububu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment