Pages

Pages

Tuesday, April 07, 2015

Mkurugenzi wa Hali ya Hewa Mstaafu Mzee Mohamed Mhita afariki Dunia

ALIYEWAHI kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dr Mohamed Mhita, amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam, baada ya kuugua kwa muda mfupi.
 Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya Makete, Mheshimiwa Muhingo Rweyemamu, kushoto aliyesimama, akisalimiana na Dr Mohamed Mhita, kulia, aliyesimama katika Tamasha la Handeni Kwetu mwaka 2013, Uwanja wa Azimio, wilayani Handeni, mkoani Tanga. Mzee Mhita, amefariki Dunia, usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.
Marehemu Dr Mohamed Mhita aliyesimama enzi za uhai wake alipokuwa katika majukumu ya Kitaifa, kama Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

Taarifa za kifo cha Mzee Mhita zilianza kuenea saa tisa za usiku, ambapo watu mbalimbali walikuwa wakizifuatilia kwa kupitia vyanzo mbalimbali vya habari ili kuthibitisha juu ya habari hizo.

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Mboni Mhita, ambaye ni mtoto wa marehemu Mhita, alithibitisha juu ya taarifa ya kifo cha baba yake kilichotokea na kuacha simanzi nzito kwa wananchi, hususan wakazi wa Handeni, ambapo ndipo alipozaliwa marehemu.
“Ni kweli tumempoteza baba yetu kama taarifa hizo zinavyosema, amefariki usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam,” alisema kwa ufupi Mh Mboni.

Taarifa za kifo cha Mzee Mhita huenda zikapokewa kwa shingo upande wa wananchi wa Handeni waliokuwa na matumaini makubwa kwa marehemu juu ya kuiendeleza wilaya ya Handeni, ambapo kwa sasa msiba wake upo nyumbani kwake Masaki, jijini Dar es Salaam.

Mhita walikuwa miongoni mwa wadau wa Handeni waliokuwa na mapenzi makubwa na wilaya yao, hali iliyomfanya awe busy nayo katika kufanya mambo mbalimbali yenye kuleta dira kwa wilaya hiyo ya Handeni, mkoani Tanga.

No comments:

Post a Comment