Pages

Pages

Tuesday, December 30, 2014

Bayport yamjaza mapesa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza MUCE kutoka kwenye fao la Bima ya Elimu

Mratibu wa Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania, Ruth Bura kulia, akizungumza jambo katika makabidhiano ya hundi kwa bwana  Kennedy Kaupenda kushoto kwake, Makao Makuu ya Bayport, mapema wiki hii. Picha zote na Mpigapicha Wetu.

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM 
TAASISI ya kifedha ya inayojihusisha na mambo ya mikopo ya Bayport Tanzania, imempatia Sh Milioni tatu mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu kishiriki cha Mkwawa (MUCE), Kennedy Kaupenda, kufuatia huduma mpya ya Bima ya Elimu inayoendeshwa na taasisi hiyo nchini.

Huduma hiyo mpya ya Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania ilianza mapema mwaka huu kwa ajili ya kuwapatia fursa wanafunzi kuendelea na masomo baada ya mzazi aliyejiunga na huduma hiyo kufariki Dunia.

Mwanafunzi wa MUCE, Kennedy Kaupenda kushoto, akizungumza baada ya kukabidhiwa hundi yake ya Sh Milioni 3 kutoka kwenye Bima ya Elimu inayoendeshwa na Bayport. Kulia kwake ni Mratibu wa Bima hiyo, Ruth Bura.   

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Bima ya Elimu inayotolewa na Bayport Tanzania, Ruth Bura, alisema Kaupenda alitajwa kama mnufaika kwa mzazi wake aliyefariki Dunia, hivyo waliamua kumtafuta kwa ajili ya kumpatia mafao yake kwa ajili ya kuendelea kupata elimu bila vipingamizi vyovyote.

Alisema huduma hiyo ina vipengele vine ambavyo ni Bronze, Gold, Silver na Exucutive, huku akisema kuwa makato ya kila mwezi ya Bronze ni Sh 2,500, ambapo fao lake ni Sh Milioni 3, wakati makato ya Gold ni Sh 6,250, huku fao lake likiwa ni Sh 7,500,000.
Ruth Bura, Mratibu wa Bima ya Elimu Bayport Tanzania kulia akimkabidhi hundi bwana Kennedy Kaupenda kwa ajili ya kuendelea na masomo ya elimu ya juu baada ya kufariki mzazi wake.


Mratibu wa Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania, Ruth Bura, kulia akizungumza jambo baada ya kumkabidhi Kaupenda hundi ya Sh Milioni 3 kutoka kwenye huduma hiyo mpya iliyoanzishwa kwa ajili ya kukamilisha ndoto za elimu kwa uwapendao.

“Pia tunacho kipengele cha Silver ambapo makato yake kwa mwezi ni Sh 3,800, huku mteja akilipwa fao la Sh Milioni 4,500,000 na kipengele cha Executive kikihusisha makato ya Sh 9,000 na kumpatia mteja fao la Sh 10,800,000, huku tukiamini kuwa huduma hii ni sehemu ya kuhakikisha kuwa Watanzania wanawawekea ulinzi wa elimu watoto wao na yoyote wanayemchagua wao,” alisema Ruth.

Akizungumzia fao hilo, Kaupenda alisema hakuwa na imani kuwa angesoma vizuri baada ya baba yake kufariki, ila baada ya kutafutwa na Bayport na kutaarifiwa juu ya mafao hayo, amepata nguvu mpya.

Kennedy Kaupenda akitafakari baada ya kuiona hundi iliyoandaliwa kwa ajili yake kutoka Bayport Tanzania juu ya fao la Bima ya Elimu.
“Nasikitika sana baba kwa kunificha juu ya kujiunga na huduma hii sambamba na kuwa mkopaji wa Bayport, hata hivyo namshukuru kwasababu fedha hizi zimekuja kunipa mwanga mpya wa kuhakikisha kuwa nasoma kwa bidii, nikiamini kiasi cha Sh Milioni tatu kitaniweka katika wakati mzuri mno,” alisema Kaupenda, huku akiwasisitiza wazazi kujiunga kwenye huduma hiyo kwa manufaa ya familia zao.

Mbali na huduma hiyo ya Bima ya Elimu kwa uwapendao, pia Bayport inajihusisha na mikopo kwa watumishi wa umma na kampuni zilizoidhinishwa, ambapo mwishoni mwa mwaka 2014 walizindua huduma ya Mikopo ya Bidhaa, ambapo bidhaa za bodaboda aina ya Lifan, Toyo na Boxer zinakopeshwa kwa wateja wa Bayport Tanzania.

No comments:

Post a Comment