Pages

Pages

Tuesday, July 01, 2014

Shindano la urembo la Qs lawekewa mikakati


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

KAMPUNI ya Qs Mhonda J  Entertainment, imesema inaweka mikakati kabambe ili shindano lao la urembo la Qs Queen linafanyika kwa mafanikio.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Joseph Mhonda, alisema kwamba mipango hiyo inakwenda sambamba na hamu ya kuona tasnia hiyo ya urembo inapiga hatua.

Alisema lengo la kuanzisha kwa shindano hilo ni kutafuta fursa za ajira mpya kwa mabinti watakaoshiriki shindano hilo lenye tija kwa watu wote.

“Shindano la Qs Queen lilifanyika mwaka jana, lakini likasimama kwa muda, hivyo nia yetu ni kujipanga ili lifanyike tena kwa mafanikio makubwa.

“Naamini wadau wote wanatumia wakati huu kuweka mikakati ya aina yake ili shindano lifanyike kwa mafanikio makubwa, licha ya changamoto mbalimbali kujitokeza,” alisema Mhonda.

Kampuni hiyo inajihusisha na kazi mbalimbali, ikiwamo kuwasimamia wasanii nyota, akiwamo Ney wa Mitego, H Baba na wengineo wanaotamba Tanzania.


No comments:

Post a Comment