Pages

Pages

Saturday, July 05, 2014

Mbeya City: Tumeanza mazozi rasmi



NA KAMBI MBWANA, DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa timu ya Mbeya City, Juma Mwambusi, amesema kwamba wameanza mazoezi rasmi kwa ajili ya kujiandaa na Ligi ya Tanzania Bara msimu ujao utakaoanza baadaye mwezi ujao.

Jana jijini Mbeya, timu hiyo iliyomaliza ligi kwa kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi inaingia uwanjani kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Prisons, zote za jijini humo.
Akizungumzia mazoezi hayo, Mwambusi alisema kwamba ameanza rasmi patashika ya kuandaa timu yao kwa ajili ya kujiandaa na Ligi ijayo.

Alisema wanaamini mazoezi yao yatakuwa na tija juu ya kuiweka sawa Mbeya City ili ijiweke katika mazingira mazuri ya kiushindani. "Naamini huu ni wakati wa kuiandaa vyema Mbeya City ili msimu ujao uanze kwa mafanikio na hatimae vijana kufanya vizuri uwanjani.

“Tumeanza rasmi mazoezi, huku tukijipanga kuwapatia burudani kamili ya soka wakazi wa Mbeya na Tanzania kwa ujumla,” alisema Mwambusi.
Mkoa wa Mbeya sasa umepata ushindani wa kisoka, huku timu za Mbeya City na Prisons zikiingia katika ushindani wa aina yake, kama timu pinzani.

No comments:

Post a Comment