Allan Kalinga-CEO for Afro-Euro Management Co. LTD
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAIMBAJI kutoka nchi tano katika Kanda ya Afrika Mashariki hadi kufikia
mwisho wa mwaka huu wanatarajiwa kushiriki katika shindano jipya la
uimbaji liitwalo Shindano la Waimbaji wa Afrika Mashariki.
Shindano
hilo ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Afro-Euro Events Management Co.
Limited, linatarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam, na kuhusisha
wasanii nguli kutoka Uganda, Tanzania, Kenya, Rwanda na Burundi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Afro-Euro Management Co. LTD,
Allan Kalinga, ambaye kwa sasa makazi yake yako nchini Uingereza,
alisema kwamba wagombea husika watachuana kuwania tuzo ya heshina ya
juu kuvikwa taji la muimbaji bora wa eneo la Afrika Mashariki.
"Umma wa Afrika Mashariki utahusishwa kuanzia mwanzo wa shindano
hili hadi mwisho na hivyo mshindi atakayepatikana atakuwa chaguo la
kweli la watu wa Afrika Mashariki, " alisema Kalinga.
MCHAKATO WA UTEUZI
Kalinga aliendelea kusema zaidi kwamba kila nchi shiriki itafanya
uteuzi wake wenyewe kuwatambua wanamuziki wake watano bora ambao
watawakilisha katika fainali ya kikanda.
Pages
▼
Pages
▼
Wednesday, July 30, 2014
Fiesta kuanzia Mwanza Agosti 9
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAKAZI na wananchi wa jijini Mwanza, Tanzania, watapata fursa
ya kuwa wa kwanza kushuhudia burudani za tamasha la muziki la Fiesta,
litakaloanza Agosti 9, CCM Kirumba, Mwanza.
Kuzinduliwa kwa tamasha hilo, ni harakati za mwendelezo wa
ziara za mikoani, ambapo wasanii mbalimbali wenye majina yao hupata nafasi ya
kupanda jukwaani kutoa burudani.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Utafiti
na Matukio, Ruge Mutahaba, alisema kwamba maandalizi ya mwisho yanafanywa ili
kuliweka pazuri tamasha hilo.
“Fiesta ni tamasha kubwa ambalo mashabiki nchini kote
wanaliheshimu na kuona ni sehemu muafaka ya kupata burudani kabambe.
“Kwa mwaka huu wadau wa muziki wa jijini Mwanza watakuwa wa
kwanza kuangalia maudhui na mikakati kabambe ya kuliweka juu tamasha hili
linalotamba Tanzania,” alisema.
Wasanii mbalimbali nchini wanajiandaa kwa tamasha hilo,
ambalo mara zote limekuwa eneo muafaka la kuwatangaza wasanii ndani na nje ya
jiji la Dar es Salaam.
Sunday, July 27, 2014
Yusuf Manji avunja Kamati ya Utendaji, aunda mpya, Ridhiwan Kikwete awekwa kando
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji, amevunja Kamati
ya Utendaji kuanzia Julai 31 na kuunda mpya kwa ajili ya kusimamia na
kuiendeleza klabu hiyo yenye maskani yake jijini Dar es Salaam.
Yusuf Manji, pichani.
Mbali na kuvunjwa kwa Kamati ya Utendaji, pia Manji
ametangaza kuzivunja Kamati zote, ikiwamo ile ya kusimamia Jengo la Mafia,
ambalo lilikuwa likisimamiwa na Mwenyekiti wake Ridhiwan Kikwete.
WAJUMBE WAPYA WA Kamati
ya Utendaji ya YANGA ni hawa WAfuaTAO:
1. Bw.Abubakar Rajabu - Mradi wa Jangwani City
2. Bw.Sam Mapande -
Sheria
na Utawala Bora
3. Bw.George Fumbuka - Uundwaji wa Shirika
4. Bw.Waziri Barnabas - Vibali vya Hatimiliki na Mahusiano
na
Wafadhili
5.Bw.Abbas Tarimba - Mipango na Uratibu
6. Bw.Isaac Chanji na
Bw.Seif Ahmed - Uendelezaji wa
Mchezo
7. Bw.Musa Katabalo - Mauzo ya Bidhaa
8. Bw.Mohammed Bhinda - Ustawishaji wa Matawi
9. Bw.David Ndeketela Sekione - Uongezaji wa Wanachama
10. Bw.Mohammed Nyenge - Utangazaji wa Habari, Taarifa,
Matangazo n.k.
Wajumbe wa Kamati
ya Utendaji iliyoundwa upya watasimamia kimsingi kamati ndogo zifuatazo:
·
Kamati ya Maadili - Bw.Sam Mapande
·
Kamati ya Nidhamu - Bw.Sam Mapande
·
Kamati ya Uchaguzi - Bw. Sam Mapande
·
Kamati ya Uchumi na Fedha - Bw.George Fumbuka
na Bw.Waziri
Barnabas
·
Kamati ya Mashindano - Bw.Seif Ahmed & Bw.Isaac
Chanji
·
Kamati ya Soka la Vijana na
Wanawake - Bw.Seif Ahmed &Bw.Isaac Chanji
·
Kamati ya Ufundi - Bw.Seif Ahmed &Bw.Isaac Chanji
5. Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wa
YANGA wanamategemeo makubwa kuwa waliotajwa
hapo juu watahakikisha wana timiza malengo yaliyokusudiwa
na YANGA ili“DAIMA
MBELE, NYUMA MWIKO” mpaka hapo itakapoamuliwa kubadilishwa au
kutenguliwa vinginevyo.
6.
Mwisho,tunawaomba
ushirikiano wa dhati ili kuhakikisha kuwa YANGA inapiga hatua mbele na inafanikiwa
katika kufikia malengo na mipango yake ya
maendeleo ya muda mfupi na ya muda mrefu kwa manufaa ya Klabu,
Timu na wana YANGA popote walipo duniani.
Pata picha mbili kali Rais Kikwete, Waziri Pinda walipokwenda kufuturu kwa Makamu wa Rais, Dkt Gharib Bilal
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, wakiongozana na mwenyeji wao Makamu
wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilali, wakati wakiwasili nyumbani kwa
Makamu kwa ajili ya kushiriki katika halfa ya futari waliyoandaliwa na
Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali katika makazi yake Oysterbay
jijini Dar es salaam juzi Ijumaa jioni Julai 25, 2014. Picha na OMR
Bunge la Katiba lazidi kukaliwa kooni
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akitoa tamko kuhusu Bunge la Katiba litakaloanza Agosti 5, 2014 ambapo walishauri Bunge hilo likae wiki mbili badala ya miezi miwili kama ilivyopangwa ili kupunguza matumizi makubwa ya fedha za Umma. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Kamati na Uongozi Jukata Omar Ali Omar, Meneja Habari na Mawasiliano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Kenny Ngomuo, Makamu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda na Mratibu wa Jukata, Diana Kidara.
Makamu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda, akisoma tamko hilo.
Thursday, July 24, 2014
Kumekucha tamasha la Saba la Muziki wa Cigogo 2014
Na Andrew Chale, Dodoma
SHAMRA
shamra za tamasha la Muziki wa Cigogo zitatarajia kulipuka hiyo kesho Julai 25,
kwenye kijiji cha Chamwino Ikulu, Mkoani hapa kwa kushuhudia vikundi zaidi ya
30, vikiwasha moto wa ngoma na muziki wa kitamaduni hu ku Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema
Nchimbi akitarajiwa kulifungua rasmi.
Katika kukuza
na kuendeleza sanaa nchini, tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu ni la msimu wa Saba
(7) likifahamika kama (Wagogo music festival 2014) lenye kauli mbiu
‘Utamaduni na Amani’ linatarajia kulindima kwa siku tatu, Julai 25 hadi
27, Kijijini hapo Chamwino Ikulu.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika mkutano
uliofanyika mapema leo kwenye ukumbi wa Maktaba ya Mkoa wa Dodoma, Mkurugenzi
mkuu wa tamasha hilo, Dk. Kedmon Mapana, wa Kituo cha Sanaa Chamwino
(Chamwino Arts Center-CAC) alisema jumla ya vikundi 31 vinatarajiwa
kushiriki tamasha hilo.
“Tamasha
la Wagogo mwaka huu ni la saba, ambapo shamrashamra ya tamasha hilo zinatarajia
kuanza majira ya saa nane mchana Mkuu wa Mkoa atakapolifungua rasmi huku
tukitaraji pia kuwa na wageni wasiopungua 1000” alisema Dr. Kedmon Mapana.
Na kuongeza
kuwa, kituo hicho cha CAC kimekuwa
kikiandaa tamasha hilo kila mwaka huku lengo kuu likiwa ni kudumisha mila na
tamaduni za Wagogo.
Taasisi ya Handeni Kwetu Foundation kuzinduliwa August 5
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SIKU chache baada ya kusajiliwa rasmi chini ya Wizara ya Maendeleo
ya Jamii, Jinsia na Watoto, Taasisi inayojulikana kama Handeni Kwetu
Foundation, imepangwa kuzinduliwa August 5 mwaka huu, katika Ukumbi wa Vijana
Social Hall, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kutafuta namna ya kusaidiana na
serikali katika mambo mbalimbali, ikiwamo Kujenga uwezo kwa jamii kujikwamua
kiuchumi na kuhamasisha utawala.
Akizungumza hilo, jijini Dar es Salaam, Msemaji wa taasisi hiyo,
Kambi Mbwana, alisema taasisi hiyo imeanzishwa na itafanya kazi zake bila
kuvunja masharti yaliyowekwa na serikali ili kuhakikisha kuwa malengo
yaliyokusudiwa yanapatikana.
Alisema kuwa taratibu za kuelekea kwenye uzinduzi huo zinaendelea
kuwekwa katika hali ya kukutana pamoja kwa wageni walioalikwa kushuhudia
uzinduzi huo wa aina yake.
“Kwa miezi kadhaa sasa taasisi ilikuwa kwenye mchakato wa usajili
wake, hivyo baada ya kukamilika, kinachofuata sasa ni kuzindua ili ianze kazi
zake kama ilivyokusudia.
“Taasisi hii itakuwa na Makao yake Makuu wilayani Handeni, lakini
itafanya kazi zake nchi nzima na huko mbele itakuwa na ofisi katika kila eneo
itakaloona inafaa,” alisema.
Sababu nyingine za kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kuleta ustawi
kwa jamii katika njanya mbalimbali, kutoa mafunzo kuhusu kilimo bora na jinsi
ya kutafuta masoko, kutoa elimu ya uraia na kuhamasisha misingi ya utawala
bora, kutoa elimu na ushauri kuhusu mbinu bora za kuimarisha afya na elimu ya msingi kuhusu Virusi vya
Ukimwi na Ukimwi.
Malengo mengine ni kutoa elimu kuhusu makundi rika katika elimu ya
uzazi, kuhamasisha na kushawishi jamii kuzingatia ustawi wa mtoto katika jamii,
kufanya utetezi kwa makundi maalum ambayo haki zao zinakiukwa na kufanya tafiti
mbalimbali zenye malengo ya kuboresha maisha ya jamii, kiuchumi na kijamii.
Semina ya kuelimisha jamii kuhusu Ukimwi yafana
Afisa
Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias
akitoa mada kuhusu tabia hatarishi zinazochangia maambukizi mapya ua VVU
kwa Vijana katika warsha ya siku tatu ya Mradi wa SHUGA Redio
inayofanyika katika Kituo cha Redio cha Nuru FM mjini Iringa.
Na Mwandishi wetu
Idadi
kubwa ya Vijana hususan wa kike wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24
wanaanza kufanya mapenzi katika umri mdogo jambo ambalo linaashiria
hatari ya maambukizi ya VVU ikilinganishwa na idadi ya Vijana wa Kiume.
Akitoa
mada kuhusu tabia hatarishi zinazochangia maambukizi mapya ua VVU kwa
Vijana katika warsha ya siku tatu ya Mradi wa SHUGA Redio inayofanyika
katika Kituo cha Redio cha Nuru FM mjini Iringa, Afisa Mradi wa Elimu ya
Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias, amesema hadi sasa
kuna Asilimia 3.9 ya wasichana wenye umri huo wamepata maambukizi ya
VVU ikilingaishwa na asilimia 1.7 ya wavulana.
Kufanya
mapenzi pia katika umri mdogo kunachangia kwa kiasi kikubwa mimba za
utotoni na kuathiri ustawi wa maisha ya wasichana. Wastani wa watoto wa
kike 6,000 huachishwa masomo kila mwaka kutokana na mimba za utotoni.
Kutana na damu changa iliyotangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Nkenge (Chadema)
JOTO la kisiasa nchini kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 limezidi kushika kasi baada ya kijana, Edson Joel, kuonyesha nia ya kuwania Ubunge katika Jimbo la Nkenge, akitaka kujitosa kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Edson Joel pichani akiwa kwenye moja ya majukumu ya kichama jimboni Nkenge.
Edson Joel mwenye kofia akiwa na timu katika moja ya shughuli za kijamii jimboni Nkenge.
Joel ameweka kambi yake ya wiki tatu jimboni humo akishiriki katika kazi mbalimbali za kijamii kwa ajili ya kuangalia namna ya kuwaingilia jimboni humo na lengo lake la kuwatumikia Watanzania, hususan wa Jimbo la Nkenge kutimia.
Joel aliuhakikishia mtandao wa Handeni Kwetu Blog kuwa anazo sifa na nguvu ya kuwatumikia Watanzania kwa kupitia chama chake cha Chadema. Habari mbalimbali juu ya siasa na wanasiasa Tanzania zitaendelea kukujia live...
Edson Joel pichani akiwa kwenye moja ya majukumu ya kichama jimboni Nkenge.
Edson Joel mwenye kofia akiwa na timu katika moja ya shughuli za kijamii jimboni Nkenge.
Joel ameweka kambi yake ya wiki tatu jimboni humo akishiriki katika kazi mbalimbali za kijamii kwa ajili ya kuangalia namna ya kuwaingilia jimboni humo na lengo lake la kuwatumikia Watanzania, hususan wa Jimbo la Nkenge kutimia.
Joel aliuhakikishia mtandao wa Handeni Kwetu Blog kuwa anazo sifa na nguvu ya kuwatumikia Watanzania kwa kupitia chama chake cha Chadema. Habari mbalimbali juu ya siasa na wanasiasa Tanzania zitaendelea kukujia live...