Pages

Pages

Monday, June 23, 2014

Taifa Stars kuelekea kesho Botswana kuweka kambi ya wiki mbili

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

TIMU ya Taifa (Taifa Stars), inaondoka kesho alfajiri kuelekea nchini Botswana kuweka kambi ya wiki mbili kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Msumbiji.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema kwamba maandalizi kwa ajili ya safari ya Stars yamekamilika.

Alisema timu hiyo itaweka kambi Botswana kwa wiki mbili kabla ya kurudi Tanzania, ambapo watakuwa wamejiweka sawa kuvaana na Msumbiji.

“Kila kitu kipo sawa kwa ajili ya safari ya Stars ambayo vijana wataweka kambi ya wiki mbili, huku tukiamini kuwa yatakuwa mazoezi mazuri.

“TFF na Watanzania wote tunadhani huu ni wakati muafaka kwetu kuiwekea mazingira mazuri Taifa Stars ili iweze kuonyesha soka zuri,” alisema.

Kwa mujibu wa Wambura, Taifa Stars itaondoka kesho alfajiri na Shirika la Ndege la Afrika Kusini kwa ajili ya kuelekea nchini Botswana kuweka kambi ya wiki mbili.

No comments:

Post a Comment