Pages

Pages

Sunday, June 08, 2014

Mzee Small kuzikwa kesho saa 10 jioni Tabata Segerea, jijini Dar es Salaam



Na Rahim Kambi, Dar es Salaam
MUIGIZAJI maarufu hapa nchini Said Ngamba (Mzee Small), amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu. 


Mzee Small pichani enzi za uhai wake, atazikwa kesho saa 10 jioni katika makaburi ya Tabata Segerea. Akizungumzia hilo, Mwenyekiti wa Chama Cha Waigizaji Tanzania mkoani Dar es Salaam, Kaftan Masoud, aliwataka wasanii kujitokeza kwa wingi katika msiba wa mkongwe huyo kisanaa.

Alisema kuwa msanii huyo amefariki na kuendeleza simanzi kwa wadau wa sanaa Tanzania kutokana na kifo cha mkongwe huyo hapa Tanzania.

“Tunaomba wasanii na wadau wote kujitokeza kwa wingi katika msiba wa mzee Small, maana kifo chake ni pigo katika tasnia ya sanaa Tanzania,” alisema.

Mzee Small amefariki siku chache baada ya kusafirishwa nchini Kenya mwili wa George Tyson aliyefariki kwa ajali ya gari akitokea Dodoma kuja jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment