Pages

Pages

Tuesday, June 10, 2014

Mshindi ‘Twenzetu Brazil’ apatikana



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMPUNI ya New Habari 2006 Ltd inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Rai, Bingwa, Dimba na The African, jana ilimtangaza Wilbert John mwenye miaka 41, kushinda shindano la Twenzetu Brazil kushuhudia mechi ya Kombe la Dunia.

Shindano hilo liliyokuwa ikiendeshwa kupitia magazeti ya Bingwa na Dimba, mshindi huyo alipatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyofanyika katika Ofisi za New Habari, Sinza, Kijiweni.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Maendeleo na Miradi wa New Habari, Michael Budigila, alisema kampeni hiyo ilidumu kwa muda wa miezi miwili na kushirikisha wasomaji wa Bingwa na Dimba kwa kutuma kuponi zilizopo kwenye magazeti hayo.

Budigila aliwataja washindi wa zawadi nyingine ambao ni Amina Shabani kutoka Mabibo aliyejishindia TV bapa pamoja na king’amuzi na simu ya mkononi ya Smartphone.

Wengine waliojishindia Smartphone katika droo hiyo ni Emma Gasto kutoka Mbezi na Juma Seleman kutoka Sumbawanga, Abasi Amiri na Elisha Yohana pia walijishindia TV bapa huku Zaituni Mussa akijishindia fedha taslimu sh. Milioni 1 na Frank Jackson kutoka Morogoro akijinyakulia pikipiki.

Kampuni ya New Habari (2006) Limited, iliandaa shindano hilo ili kuwapa fursa Watanzania kuweza kushiriki na watu wengine duniani furaha ya mchezo wa soka, unaochezwa na kupendwa na watu wengi duniani kwa kwenda Brazil au kuangalia kupitia luninga watakazoshinda.

Aidha shindano hilo lililenga kuwapa hamasa vijana wa kike na wa kiume kushiriki katika mchezo wa mpira wa miguu, kupitia Kombe la Dunia ambalo ni tukio kubwa la kimichezo linalotokea kila baada ya miaka minne.











No comments:

Post a Comment