Pages

Pages

Sunday, May 04, 2014

Wazee wa Ngwasuma hapatoshi leo Njombe



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya FM Academia, Wazee wa Ngwasuma, leo inafanya shoo ya nguvu katika Ukumbi wa Turbo, uliopo mjini Njombe.

Shoo hiyo itakuwa ya mwisho kwa bendi hiyo iliyokuwa katika ziara ya mikoani, ambapo walipitia katika mikoa mbalimbali, wakianza Mkoa wa Morogoro, Jumatano iliyopita.

Akizungumza kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa bendi hiyo, Kelvin Mkinga, alisema kuwa shoo hiyo itakuwa ya aina yake kwa mshabiki wa Njombe.

“Tumekuwa na kawaida ya kufanya ziara ya mara kwa mara katika mikoa Tanzania, hivyo kesho (leo), mashabiki wa Njombe wataona kwanini sisi tupo kileleni.

“FM Academia ni miongoni mwa bendi imara na zenye mashabiki wengi sambamba na mikakati ya kuendelea kutesa kileleni,” alisema.

Wazee wa Ngwasuma wapo chini ya Nyosh El Saadat, akishirikiana kwa karibu na wakali kibao, akiwamo Patchou Mwamba, Pablo Masai, Totoo Kalala na wengineo.

No comments:

Post a Comment