Pages
▼
Pages
▼
Tuesday, May 06, 2014
Super D afagilia CD zake za masumbwi
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KOCHA wa masumbwi hapa nchini, Rajabu Mhamila, Super D, amesema kwamba kutengeneza kwake CD mbalimbali za mchezo huo kumezidisha hamasa ya vijana kujiingiza katika ngumi pamoja na kutoa ujuzi kwa mabondia nchini.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mhamila alisema kwamba wazo la kuanzisha utaratibu huo wa kuandaa CD za ngumi limeleta mafanikio makubwa kwa wadau wote.
Alisema ataendelea na utaratibu wa kuandaa CD za ngumi zinazokutanisha mabondia mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kuibua hamasa nzuri kwenye ulingo wa masumbwi.
“Vijana wengi wanaofanikiwa kuangalia CD zangu za masumbwi nao wanapata elimu kubwa na hamasa kwa ajili ya kufanya bidii ili wawe mabondia mahiri.
“Naamini suala hili kwangu ni moja ya mafanikio, huku nikiamini kuwa nitaweka mkazo katika uandaaji wake ili wazo hili liwe na tija kwa mabondia na wale wasiokuwa mabondia,” alisema.
Mbali na kuandaa CD hizo, Mhamila pia ni kocha wa ngumi katika klabu ya Ashanti Boxing Club, yenye maskani yake jijini Dar es Salaam, ikiwa na vijana wenye ndoto za kuwika Kimataifa.
No comments:
Post a Comment