Pages

Pages

Saturday, May 17, 2014

Mwili wa marehemu Adam Kuambiana wahifadhiwa Muhimbili, kikao cha dharula cha wadau na wasanii kufanyika Leaders Club



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWILI wa marehemu Adam Kuambiana umehamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, huku kikao cha wasanii na wadau kikitarajiwa kufanyika muda huu katika Viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam.
Marehemu Adam Kuambiana, pichani, enzi za uhai wake.
Kuambiana aliyetamba na filamu kadhaa, ikiwamo ile ya Regina iliyotungwa na msanii Jacob Stephen JB, alifariki mapema leo wakati anawahishwa katika Hospitali ya Mama Ngoma Mwenge, jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Sherehe na Vifo wa Chama Cha Waigizaji Tanzania, Dastan Masoud aliuambia Mtandao huu kuwa mwili wa msanii huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili.

“Muda huu tumetoka kuuhifadhi mwili wa Kuambiana Muhimbili, hivyo tunaelekea Leaders kufanya kikao cha dharula kwa ajili ya kuutafakari msiba huu mzito,” alisema.

Kifo cha Kuambiana kimepokewa kwa majonzi ikiwa ni siku moja baada ya msiba mwingine wa mwimbaji wa muziki wa dansi, Amina Ngaluma kutokea nchini Thailand.

No comments:

Post a Comment