Pages

Pages

Saturday, May 24, 2014

HANDENI KWETU FOUNDATION


HABARI za leo mabibi na mabwana, hususan wadau na member wa group la Handeni Kwetu, linalopatikana katika ukurasa wa facebook. Awali ya yote napenda kumshukuru Mungu kwa kutupigania, maana ametupa pumzi na afya.
 Upande wa mbele wa Katiba ya Handeni Kwetu Foundaation unavyoonekana.
Aidha niwashukuru wadau wote tunaoendelea kushirikiana kwa namna moja ama nyingine, wakiwamo wadau wote wa group na marafiki zetu katika mitandao ya kijamii.

Mara kadhaa nimekuwa nikipata maswali yanayoulizia dhamira ya kukutana pamoja au kuanzisha kundi litakalokuwa na maana ya kusaidiana wanachama na Watanzania wote, hususan wakazi na wananchi wa Handeni na mkoa mzima wa Tanga.
 Adam Malinda, mmoja wa waasisi wa Handeni Kwetu Foundation, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti, akifurahia jambo katika moja ya vikao vya kujadili kuasisiwa kwa taasisi hii. Kulia ni Mengi Ibrahim Mabewa, ambaye ni muasisi, akiwa kwenye kikao.
Kikao kinaendelea, kulia ni Daud Aidano, mwanachama mwanzilishi.

Maswali ya aina hii tumekuwa tukiyajibu na kuafikiana. Tulichogundua, baadhi ya wadau wanapenda kufanya kazi kwa kushirikiana. Kutoa mawazo yao kwa ajili ya maendeleo yao.
Hata hivyo, kusajili kundi kulikuwa na ugumu wake, maana litakuwa na ukomo wa utendaji wake wa kazi. Ni kutokana na hilo, kwa pamoja, tunayo furaha kusema kuwa kumeanzishwa taasisi inayokwenda kwa jina la Handeni Kwetu Foundation.

Hadi wakati huu, kila kitu kimekwenda vizuri. Hii ni baada ya kukutana kwanza wachache wao, wakafanya vikao mbalimbali, wakaandika Katiba yao, kasha wakaenda Handeni kuomba barua ya utambulisho, kabla ya kuelekea Wizarani kwa usajili.

Haya yote yameshafanyika. Ushirikiano tuliupata kwa kila eneo tulipofika, jambo ambalo limeendelea kufanikisha mchakato huu. Ndugu zetu, sote tunapenda kushirikiana.


Tunapenda kusaidiana na serikali pamoja na viongozi wao. Sisi tunaamini tutafanya kazi kwa nafasi yetu kwa kushirikiana na watu wote, ikiwamo serikali na viongozi wake kwa ujumla.
Ingawa taasisi hii inaitwa Handeni Kwetu Foundation, ila itafanya kazi sehemu mbalimbali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ndiyo Makao Makuu yake yatakuwa Handeni, ila kutakuwa na ofisi kila sehemu itakapoonekana inafaa, ikiwamo jijini Dar es Salaam.

Taasisi hii itakuwa na wanachama na itajiendesha kwa kufuata sheria zote zilizowekwa kwa mujibu wa Katiba mama na Katiba ya Handeni Kwetu Foundation.

DIRA

Lengo Kuu la asasi hii ni kujenga uwezo kwa jamii kujikwamua kiuchumi na kuhamasisha utawala bora.

DHAMIRA

3.2.1 Kuleta ustawi kwa jamii katika nyanja mbalimbali.

MADHUMUNI

3.2.0 Kutoa mafunzo kuhusu kilimo bora na jinsi ya kutafuta masoko.
3.2.1 Kutoa elimu ya ujasiriamali katika vikundi mbalimbali.
3.3.3 Kutoa elimu ya uraia na kuhamasisha misingi ya utawala bora.
3.3.4 Kutoa elimu na ushauri kuhusu mbinu bora za kuimarisha afya, na elimu ya msingi kuhusu Virusi vya Ukimwi na Ukimwi.
3.3.5 Kutoa elimu kuhusu makundi rika katika elimu ya uzazi.
3.3.6 Kuhamasisha na kushawishi jamii kuzingatia ustawi wa mtoto katika jamii
3.3.7 Kufanya utetezi kwa makundi maalum ambayo haki zao zinakiukwa.
3.3.8 Kufanya tafiti mbalimbali zenye malengo ya kuboresha maisha ya kijamii na kiuchumi.

Viongozi wa taasisi hii wapo tayari kufanya kazi na wananchi wote kama ilivyoelezwa kwa ajili ya kufanikisha adhma ya kuanzishwa kwa asasi hii. Taasisi hii imezaliwa kwenye group la Handeni Kwetu, ila haina uhusiano wa moja kwa moja na kundi hili.

Mtu yoyote anaweza kuwa member wa kundi la Handeni Kwetu au taasisi. Si lazima mtu anayekuwa mwanachama wa group basi pia akawa mwanachama wa taasisi ya Handeni Kwetu Foundation.

Baada ya kukamilika kwa baadhi ya mambo, basi tutaanza kushughulikia taratibu za uzinduzi wa taasisi au vyovyote itakavyoonekana inafaa. Kuna mengi ya kusema, ila tutaendelea kupeana habari, kama mwendelezo wa kuanzishwa kwa taasisi hii.

Pia wanaotaka kujiunga na taasisi hii kama wanachama watapaswa kufuata taratibu zitakazowekwa, ikiwa ni baada ya kuisoma Katiba na kuielewa pia. Tunaangalia uwezekano pia wa kuiweka Katiba kwenye blog na website ili kila mmoja aisome na kuielewa kabla ya kuwa mwanachama.

Baada ya kukamilisha baadhi ya mambo, tutatoa taarifa wapi ofisi hii inapatikana katika mitaa ya wilayani Handeni kama Makao Makuu na ofisi nyingine za mikoani, japo haitakuwa kwa haraka. Ndugu, sababu ya kuanzishwa kwa taasisi hii imeelezwa hapo juu.

Tunaomba wadau wote tuendelee kushirikiana. Na wale waliokuwa wanapendekeza kusajiliwa kwa kundi hili, basi ni wakati wao kujiunga na taasisi wawe wanachama ili yale malengo yao ya kujitolea katika jamii yatimie.

Ukiwa una maoni yoyote au unapenda tu kujifunza kutokana na taasisi hii au ukipenda kuwa mwanachama; basi unaweza kuwasiliana na viongozi wetu, leo na hata kesho taasisi itakapoanza kufanya kazi rasmi kama ilivyokusudiwa.

Sadick Mbwana-Mwenyekiti +255 653 433245, +255 686 726965
Adam Malinda- Makamu Mwenyekiti +255 784 587838
Jerome Mhando-Katibu +255 718 372741
Yasin Mohamed-Mweka Hazina +255 713 420242
Mengi Mabewa- Mwenyekiti wa Maadili, Katiba na Kanuni +255 783 502618, +255 713 502618
Sanura Ally Mpambile-Mkuu wa Utawala +255 713 766017
Kambi Mbwana-Msemaji Mkuu +255 712 053949


Baada ya kusema hayo, naomba kukushukuru tena kwa kitendo chako cha kiungwana cha kusoma andiko hili. Naomba tuendelee kushirikiana kwa namna moja ama nyingine kwa maendeleo ya Taifa letu.

Kuanzia wakati huu, tutakuwa tonatoa habari mbalimbali kwenu ili kuwajulisha hatua kwa hatua safari ya kuanza kazi kwa taasisi hii ya Handeni Kwetu Foundation.
Wako mtiifu

Kambi Mbwana, Msemaji Mkuu
Handeni Kwetu Foundation
Mei 24, mwaka 2014

No comments:

Post a Comment