Pages

Pages

Friday, March 07, 2014

Dayna: Wimbo wa ‘Mimi na Wewe’ unanipa raha hadi natamani kuvua nguo


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

MWIMBAJI wa muziki kizazi kipya, Mwanaisha Said, maarufu kama ‘Dayna’, amesema wimbo wake wa ‘Mimi na Wewe’ unampa raha anapoimba jukwaani kiasi cha kutamani kuvua nguo jukwaani.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Dayna alisema kuwa anapoimba jukwaani anapata raha zaidi, hivyo kujikuta anakuwa na nguvu kubwa na ndoto za kuwapa raha mashabiki wake katika shoo zake.

Alisema hali hiyo inamfanya aendelee kufanya vizuri jukwaani kwa kucheza na kuimba kwa hisia, hivyo wakati mwingine hutamani avue nguo.


“Unapoimba nyimbo nzuri jukwaani na inayokusisimua wewe mwenyewe, hufikia kutamani kuvua nguo, jambo ambalo linaweza kutafsiriwa vibaya na wengi.


“Kwangu mimi ninapoimba wimbo wa Mimi na Wewe hupata raha zaidi, hivyo kama najichunguza ili nisiweze kuvua nguo jukwaani na kusababisha maswali mengi,” alisema.


Dayna aliibuliwa na wimbo wake Mafungu ya Nyanya, akiimba kwa ushirikiano mkubwa na nyota wa muziki huo, Lawrence Malima, maarufu kama Marlaw.

Mwisho

No comments:

Post a Comment