Pages

Pages

Saturday, March 01, 2014

Coastal Union yaipinda Ashant United



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BAADA ya kuwanyamazisha vijana wa Mbeya City, katika Uwanja wao wa nyumbani Mkwakwani mjini Tanga, timu ya Coastal Union sasa inaiwinda timu ya Ashanti United, mchezo utakaofanyika Machi 8 mwaka huu.

Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka, itafanyika katika Uwanja wa Mkwakwani, ambapo Coastal wameipania vilivyo mechi hiyo ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Coastal, Hafidh Kido, alisema kuwa wanajiandaa vizuri kwa ajili ya kuwafunga Ashanti United, nyumbani kwao.

Alisema mechi ya Ashanti ni muhimu kwao, huku wakiamini kuwa wachezaji wao hawatafanya makosa katika kuwapa raha uwanjani.

“Tunaamini kuwa mechi itakuwa ngumu kwasababu ligi ipo katika ushindani, ila hakuna cha kupoteza, ukizingatia kuwa tuna dhamira ya kufanya vizuri katika mechi zilizosalia.

“Tunaomba wadau na mashabiki wetu waendelee kutuunga mkono kwasababu vijana wapo vizuri na hakuna cha kupoteza, dhidi ya Ashanti,” alisema.

Katika mechi iliyowakutanisha na Mbeya City, Coastal walishinda bao 2-0 na kuwashangaza wengi, hasa kwa kuangalia kiwango cha Mbeya City.

No comments:

Post a Comment