Pages

Pages

Tuesday, March 04, 2014

Bellah atua leo kutoka Ulaya, kufanya makamuzi Mango Garden akiwa na bendi yake ya Malaika


NA KAMBI MBWANA, DAR ES SALAAM

WADAU wa muziki wa dansi wanaoishabikia bendi ya Malaika, Ijumaa hii watapata fursa nyingine ya kuangalia makali ya Rais wa bendi hiyo, Christian Bellah, alirejea jana kutoka nchini Sweden.



Christian Bellah, pichani.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa bendi hiyo, Michael Loki, aliwataka wadau wao kuingia kwa wingi katika onyesho lao la Mango Garden Ijumaa hii kumuona mkali huyo mwenye uwezo wa kucheza na sauti akifanya makubwa jukwaani.


Alisema kuwa Bellah amerejea nchini akiwa na nguvu zote za kuhakikisha kuwa anafanya vizuri katika tasnia ya muziki wa danssi nchini, akiwa na bendi yake ya Malaika.

“Bellah amerejea akiwa na nguvu mpya katika kuhakikisha kuwa mambo yanakuwa mazuri kwa kuwapatia burudani kamili wadau na mashabiki wa bendi yetu,” alisema Loki.

Baada ya kuwasili nchini, Bellah alisema amewaandalia vitu vipya ambavyo watavisikia siku ya Ijumaa katika onesho la bendi yao ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni.


No comments:

Post a Comment