Pages

Pages

Thursday, March 27, 2014

Alliance wasifiwa kwa juhudi za kuendeleza michezo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKURUNGENZI  Mtendaji wa Shule  na kituo cha kukuza michezo ya vijana cha Alliance School Sports Academy, James Bwire amesema timu ya Alliance inayotoka kituo hicho ikipanda daraja, ubigwa wa Ligi Kuu utahamia jijini Mwanza.

Akizungumza jijini Mwanza, baada ya kumalizika kwa mechi kati ya Alliance na timu ya Chuo cha Biashara (CBE), alisema vijana wanaondaliwa na kituo hicho watabadilisha soka nchini na kuleta changamoto ligu kuu.


Bwire alisema vijana wa timu ya Alliance waliopo daraja la nne hivi sasa wanaandaliwa na kupewa mafunzo ya kimichezo ngazi ya kimataifa ndio maana wanashinda  mechi zao zote ndani na nje ya nchi.


“Kituo chetu kinaandaa vijana wa michezo  kwa malengo, unajua zipo timu zinapanda daraja na kushiriki ligi kuu kwa kubahatisha na kushuka kwa muda mfupi, sisi hilo hatutaki ndio maana yapo masomo ya jinsi ya kucheza mpira uwanjani.


"Nadhani ni mara ya kwanza  nchini kuona  mtoto anayecheza ligi daraja la nne anachukuliwa hadi timu ya Taifa, lakini Alliance imefanikiwa kutoa Atanas Mdamu.

“Sasa nasema Alliance ikifanikiwa kufikia ligi kuu, itafuta uteja wa kombe kubaki Dar es Salaam, timu hii itabadilisha soka na mazoea yaliyopo sasa, hili nalisema kwa dhihiri kabisa kwani historia imeanza kujionyesha,kila timu za ndani na nje tunashinda na vikombe tunachukua.


“Tunajua kuna watu hawataki kuona timu ndogo inakuja kasi kama ilivyo Mbeya City ambayo kidogo imeleta changamoto , nawaomba viongozi wake wasiwe watu wa kurubuniwa.

No comments:

Post a Comment