Pages

Pages

Saturday, February 15, 2014

Yanga yaifuata Al Ahly Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuwafunga Komorozine bao 12-2mtandika



Na Mwandishi Wetu, Comoro
TIMU ya Yanga, imesonga mbele katika michuano ya Kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kuwatandika Komorozine, nchini Comoro leo kwa jumla ya mabao 5-2.


Mrisho Ngassa pichani.
Matokeo hayo yanawafanya Yanga wasonge mbele kwa jumla ya mabao 12-2. Mechi inayofuata Yanga itavaana na timu ngumu ya Al Ahly ya nchini Misri.

Itakuwa mechi ngumu inayosubiriwa kwa hamu, ukizingatia kuwa Yanga imefuzu kwa kucheza na timu kibonde, hivyo kwa sasa itajiandaa vizuri juu ya kuelekea kwenye pambano lao na Al Ahly.

Mabao ya leo yalifungwa na Hamis Kiiza 13, Mrisho Ngassa aliyefunga bao tatu, dakika ya 22, 87, 90, wakati Simon Msuva aliingiza bao kwenye dakika ya 37.

No comments:

Post a Comment