Pages

Pages

Wednesday, February 19, 2014

Wachoma Nyama wapigwa msasa - Mwanza

Na Mwandishi Wetu, Mwanza
KAMPUNI ya Bia Tanzania(TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari Lager jana imetoa mafunzo kwa  wachoma nyama kutoka Baa mbali mbali za Mkoa wa Mwanza ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Safari Nyama Choma kwa mwaka 2014 yatakayo fanyika katika viwanja vya Furahisha.

Jaji Mkuu wa Safari Lager Nyama Choma, Lawrence Salvi
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kanda ya Ziwa, Erick Mwayela, alisema lengo la kutoa mafunzo ni kutoa elimu kwa wachoma nyama ukizingatia uchomaji nyama ni moja  sehemu ya kujiingizia kipato katika Bar. 

Mwayela alisema kutokana na hali hiyo wakaona ni vema wakaendesha Semina kwa wachoma nyama ili waweze kukidhi vigezo vya mahitaji ya Wateja ili waweze kufurahia Nyama choma kama ilivyo kwa vyakula vingine ili kuendana na kauli Mbiu ya Bia ya Safari Lager isemayo“ Safari Lager bila nyama choma haijakamilika.”

Aliongeza kuwa baada ya mafunzo hayo yaliyotolewa kwa Baa 37 ambao wametunukiwa vyeti vya ushiriki  pia kutakuwa na mashindano ya kuchoma nyama ambapo washindi 10 watapatikana kutokana na watakaofuzu vigezo na masharti waliyopewa katika semina hiyo.

Alisema Fainali za Mashindano zitafanyika Machi 9, Mwaka huu katika Viwanja vya Furahisha ambapo washindi watapewa zawadi kuanzia mshindi wa kwanza atakayejinyakulia Shilingi Milioni moja na Kikombe, mshindi wa pili Laki nane, Mshindi wa tatu Laki 6, Mshindi wa nne laki nne na Mshindi wa Tano shilingi laki mbili huku mshindi wa Sita hadi wa Kumi watajinyakulia kifuta jasho cha shilingi 50,000/=.

Alisema namna ya kuwapata washindi ni kutokana na wateja kupiga kura katika utaratibu utakaobandikwa katika Baa shiriki ambapo mteja atapiga kura kupitia simu ya mkononi ili kuichagua baa inayochoma nyama vizuri.

Aliongeza kuwa baada ya zoezi hilo kukamilika katika Mkoa wa Mwanza itaendelea katika Mikoa mingine ambayo ni Kilimanjaro,Arusha na Dar Es Salaam, mikoa ambayo imetajwa kuwa ndiyo vinara wa uchomaji nyama pamoja na kuongoza kwa mauzo ya bia ya Safari Lager tofauti na maeneo mengine.

Kwa upande wake Mkufunzi wa Mafunzo hayo, Laurence  Salvi ambaye pia ni Jaji Mkuu wa mashindano hayo amesema huwezi kuandaa mashindano bila ya kutoa Elimu, hivyo TBL wamefikiria jambo la msingi sana lenye manufaa kwa waandaaji yaani wachoma nyama mpaka kwa watumiani yaani mlaji.
Bwana Lawrence binfsi aliishukuru TBL kupitia bia ya Safari Lager kufikiria jambo zuri la kufadhili elimu kwa kwa wachoma nyama jambo ambalo si faida kwa wachoma nyama tu bali hata watumiaji sasa watakula nyama inayostahili.

No comments:

Post a Comment