Pages

Pages

Saturday, February 08, 2014

TFF kuisaidia Zanzibar kutambuliwa FIFA



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
RAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi, amesema amepania vilivyo kuweka uhusiano mwema na Chama cha soka Visiwani Zanzibar, ikiwa ni pamoja na kuhangaikia ili wapate uanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani FIFA.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Malinzi alisema kwamba uhusiano mwema huo utakuwa na tija kwa soka la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuchanganya Bara na Visiwani.

Alisema kuwa tangu aingie madarakani, amekuwa akifanya ziara mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha uhusiano huo mwema.

“Juhudi hizi zinakwenda kwa pamoja kuhakikisha kuwa Zanzibar nao wanapata uanachama wa FIFA ili iwe chachu ya kukuza soka letu.

“Hii inawezekana kwa kuangalia faida kubwa itakayopatikana, ukizingatia kuwa kukuza soka kunahitajika ushirikiano wa jamii yote ya wapenda mpira wa miguu,” alisema.

Aidha, Malinzi pia aliwahakikishia Watanzania kuwa ndani ya uongozi wake, atatimiza kiu yake ya kila mkoa kuwa na Uwanja mzuri ili  kuwa rahisi kufanyika kwa michuano mbalimbali.

No comments:

Post a Comment