Pages

Pages

Monday, February 03, 2014

Mapacha Watatu na Akudo Impact kuachia shoo ya nguvu siku ya Wapendanao huku wakitambulisha wanamuziki wao wapya



Hapo sasa, Jose Mara, Tarsis Masela na Khalid Chokoraa wakionyesha umahiri wao wakati wananadi shoo yao ya pamoja.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BENDI za Mapacha watatu na Acudo Impact watafanya onyesho la pamoja kwenye sherehe za Siku ya wapendao katika Ukumbi wa Letas Lounge (Business Park), jijini Dar es Salaam.
Tamasha hilo la siku ya wapendanao ambalo hufanyika kila Februari 14 ya kila mwaka limepewa jina la “No biff Tupendane” litahusisha bendi mbili ili kuhakikisha wanatoa burudani ya uhakika kwa mashabiki wao siku hiyo.
Khalid Chokoraa akionjesha waandishi wa habari juu ya shoo yao ya pamoja.

Kushoto ni Meneja wa Akudo Impact, Ramadhan Pesambili, akifuatiwa na Tarsis Masela Rais wa Akudo Impact, akifuatiwa na Meneja wa Mapacha Watatu, Khamis Dakota pamoja na Mkurugenzi Khalid Chokoraa katika mazungumzo na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Mapacha Watatu, Khamid Dakota, kulia, wakati kushoto kwake ni Rais wa Akudo Impact, Tarsis Masela, wakizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja, Khamis Dakota, Jose Mara, Tarsis Masela na Khalid Chokoraa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini, Meneja wa bendi ya Mapacha watatu, Khamis Dacota alisema kuwa pia siku hiyo kila bendi itatambulisha wanamuziki wapya waliojiunga na bendi hizo.
“Lengo la bendi hizi kupanda jukwaa moja ni kufuta ile dhana iliyopo kwa wadau kuwa wasanii wa bendi hizi wana ugomvi sambamba na kutambulisha wasanii ambao wamejiunga kuongeza nguvu katika vikosi hivi”, alisema Dacota.
Pia alisema wataimba wimbo maalum kwa ajili ya siku hiyo wimbo ambao utaimbwa na bendi zote mbili kwani wameutunga kwa pamoja na wameufanyia mazoezi pamoja. Vile vile watatoa zawadi maalum kwa wale wapendanao watakao kuwa wamependeza.

Picha zote kwa hisani ya Lenzi ya Michezo Blog

No comments:

Post a Comment