Pages

Pages

Saturday, February 01, 2014

Kamwaga awaangukia wadau wa Simba



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga, amesema kwamba klabu hiyo haiwezi kupiga hatua ya juu zaidi kama watu wote hawatashirikiana katika kuangalia maendeleo yao kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga, pichani.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kamwaga alisema kuwa hili kuhakikisha kuwa maendeleo yanakuwa mazuri katika klabu yao, ni lazima wafanye kazi kwa ushirikiano baina ya viongozi, wanachama na mashabiki wao.

Alisema mara kadhaa klabu kongwe ikiwamo Simba inakuwa kwenye migogoro ya kila wakati, hali inayosababisha moyo wa uzalendo kupungua na kuwaachia viongozi peke yao jambo ambalo si sahihi.

“Ni wakati huu wa viongozi na wanachama wote kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuleta tija katika maendeleo ya mpira wa miguu hususan ndani ya klabu yetu ya Simba.

“Naamini huu ndio mpango mzuri kwa Simba na hakuna njia ya panya itakayotupatia maendeleo zaidi ya kuona watu wote tunakuwa kitu kimoja juu ya suala hili la maendeleo ya Simba,” alisema.

Kabla ya kutangazwa kuwa Katibu Mkuu, Kamwaga alifanya kazi Simba kama Ofisa Habari, nafasi ambayo kwa sasa inashikiliwa na mwandishi Asha Mhaji.

No comments:

Post a Comment