Pages

Pages

Saturday, February 01, 2014

Kamati ya Lembeli yatembelea Hifadhi ya Mkomazai


Mwenyekiti wa kamati ya ardhi, maliaasili na mazingira, James Lembeli,akisalimiana na watumishi wa hifadhi ya Mkomazi jana baada ya kamati yake kuwasili katiika hifadhi hiyo.
Mtaalamu wa wanyama, Tony Fitzjohn akimuongoza Mwenyekiti wa kamati ya ardhi, maliaasili na mazingira, James Lembeli, ndani ya hifadhi ya Mkomazi.
Mwenyekiti wa kamati ya ardhi, maliaasili na mazingira, James Lembeli (wa kwanza kulia), akimsikiliza mtaalamu wa wanyama wa hifadhi ya Mkomazi, Tony Fitzjohn, kamati hiyo ilipotembelea hifadhi hiyo juzi, kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahamud Mgimwa, pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la  Hifadhi ya Taifa, Allan Kijazi.
Kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Mazingira ikiwasili katika hifadhi ya Mkomazi iliyoko wilayani Same, Mkoani Kilimanjaro. aliyeshika Ipod ni Mumbe wa kamati hiyo, Grace Kiwelu, viti maaalum (Chadema).
Mwenyekiti wa kamati ya ardhi, maliasili na mazingira, James Lembeli akisikiliza maelekezo ya Mtaalamu wa Wanyama Tony Fitzjohn muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kwenda kutizama Faru wanahifadhiwa katika Hifadhi ya Mkomazi. nyuma yake ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahamud Mgimwa (kushoto).
Baadhi ya Mbwa mwitu wanaopatikana katika hifadhi ya Mkoamzi ambao wanadaiwa kuwa tayari kuaachiwa kuondoka nje ya mipaka ya hifadhi hiyo.
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Mahamud Mgimwa (kulia), Mwenyekiti wa kamati ya ardhi, maliasili na mazingira, James Lembeli, pamoja na mtaalamu wa wanyama, Tony Fitzjohn wakimshangaa Tembo mtoto anayetunzwa katika hifadhi ya Mkomazi. kwa mbali ni Mjumbe wa kamati hiyo, mbunge wa viti maaalum Morogoro, Susan Kiwangwa.

No comments:

Post a Comment