Pages

Pages

Friday, January 10, 2014

Wadau wajigamba kuwa Morogoro ni ngome ya Jahazi Modern Taarab, chini ya Mzee Yusuph

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKOA wa Morogoro umetajwa kama ngome ya kundi la Jahazi Modern Taarab, hali inayowafanya mashabiki wakanyagane kila linapofanya shoo mkoani humo.
Mzee Yusuph pichani, akicharaza kinanda.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mdau wa muziki wa taarabu, ambaye pia ni Mratibu wa shoo ya Jahazi iliyopangwa kufanyika Januari 31 katika Ukumbi wa Tanzanite Complex, Warda Makongwa, alisema watu wa Morogoro wanaipenda sana Jahazi.
Alisema ingawa kundi hilo pia linaheshimika katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, lakini kwa Morogoro ni miongoni mwa ngome zao hapa nchini.
“Heshima kubwa ya Jahazi imejikita kwa mkoa wa Morogoro, hivyo tunaamini kwa pamoja tutaufungua mwaka huu kwa burudani za aina yake kutoka kwa Jahazi.
“Kila kitu kipo sawa kuonyesha burudani za ukweli kutoka kwa Jahazi chini ya Mzee Yusuph, hivyo tunaomba wadau waje wka wingi katika Ukumbi wa Tanzanite,” alisema Warda.
Kwa mujibu wa Warda, maandalizi ya safari ya Jahazi kwa mkoa wa Morogoro yamekamilika, hivyo wadau wanapaswa kujiandaa na kujivunia burudani ya Jahazi.

No comments:

Post a Comment