Pages

Pages

Saturday, January 11, 2014

Mwandishi wa Habari za Michezo, Sultan Sikilo afariki Dunia


MWANDISHI wa habari za michezo Tanzania, Sultan Sikilo, mwenye nguo nyekundu mbele, amefariki Dunia jana na kuleta simanzi kubwa kwa tasnia hiyo ya habari. Taarifa za kifo chake zimepokewa kwa simanzi huku kila mmoja akishindwa kuamini masikio yake.

Kwa mujibu wa marafiki zake, msiba upo Keko na taarifa zinasema Sultan Sikilo atazikwa leo mchana, ikiwa ni kuhitimisha maisha yake ya duniani. Kwa wale watakaopenda kujumuika na wanahabari hasa chama cha TASWA saa tatu leo walitarajia kukutana viwanja vya Posta Kijitonyama, ili kuelekea msibani keko
Pumzika kwa amani Sikilo, mwandishi na mdau wa michezo.

No comments:

Post a Comment