Pages

Pages

Friday, January 03, 2014

RSK Kibajaji akamilisha wimbo Mapenzi ya Pesa


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

MSANII mwenye maskani yake Handeni, mkoani Tanga, Ramadhan Said Killo, ama RSK, amekamilisha kutengeneza wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Mapenzi Pesa’.
Msanii RSK mwenye maskani yake wilayani Handeni mkoani Tanga.
Msanii huyo anayesaka ufalme wa muziki wa kizazi kipya, akitokea Tanga kwa Wagosi wa Kaya, ni kati ya vijana wanaopigania nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.

Akizungumza jana kwa njia ya simu, msanii huyo alisema kuwa wimbo huo umetengenezwa katika Studio ya EnoBeats chini ya mtayarishaji wake Black Man.

RSK Kibajaj alisema kuwa anaamini wimbo huo utakuwa chachu ya kudhihirisha makali yake katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini.

“Nipo katika harakati za kuonyesha makali yangu katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, hivyo naamini wimbo wangu wa Mapenzi ya Pesa utakuwa njia nzuri.

“Naomba Watanzania wanipe ushirikiano juu ya wimbo wangu na kazi zangu zote ili nifanikiwe katika anga ya muziki huo, ukizingatia kuwa sanaa ndio kazi ninayoipenda,” alisema RSK Mkufu Kibajaj, mwenye maskani yake wilayani Handeni.

Nyimbo alizowahi kuachia msanii huyo ni pamoja na Kibajaji na Usiniache, ambazo bado hazijafanikiwa kutangaza makali yake nje ya wilaya hiyo, likiwamo jiji la Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment