Pages

Pages

Thursday, January 02, 2014

Minziro: Sitishwi kuachwa kwangu Yanga

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
ALIYEKUWA kocha msaidizi wa klabu ya Yanga, Fredy Minziro, amesema kwamba hatishwi na uamuzi wa kuachwa kwake katika benchi la ufundi la timu hiyo, kwasababu anaamini ujuzi wake atapata sehemu kwa kuupeleka.
Fredy Felix Minziro, aliyekuwa kocha msaidizi wa Yanga
Maneno ya Minziro yamekuja baada ya Yanga kutimua benchi lote la ufundi, ikiwa ni mwendelezo baada ya kumuacha Kocha wao Mkuu, Ernest Brandit.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Minziro, alisema kuwa amekuwa akivunja ujuzi mwingi kutoka kwa makocha mbalimbali waliopita Yanga katika kipindi cha miaka minne, huku akiwa kama kocha msaidizi.
Alisema jambo hilo linampa matumaini makubwa kuwa uwezo wake umekuwa mkubwa na hawezi kukosa timu ya kuifundisha atakapoona inafaa, hivyo hana shaka na uamuzi wa mabosi wake.
“Siwezi kuumizwa na hatua hii ya kuachwa Yanga, ukizingatia kuwa sijaona tatizo langu wala kupewa sababu ya kueleweka kwanini benchi la ufundi linaachwa bila sababu za msingi.
“Hata hivyo kwakuwa wao ndio wameamua, nimepokea uamuzi huo kwakuwa nitakapoamua kusaka timu ya kufundisha siwezi kukosa kutokana na ujuzi wangu niliyokuwa nao,” alisema Minziro.
Uamuzi wa Yanga umekuja huku ukipokewa kwa shingo upande na mashabiki wao, ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kinyang’anyiro cha mzunguuko wa pili wa ligi ya Tanz

No comments:

Post a Comment