Pages

Pages

Thursday, January 16, 2014

Rais Kikwete ashauriwa uteuzi wa Baraza la Mawaziri


Na Oscar Assenga,Tanga.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dokta Jakaya Mrisho Kikwete ameshauri kuwachagua mawaziri waledi na wazalendo ambao watahakikisha wanafanya kazi zao ipasavyo lengo likiwa ni kuharakisha maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla kwa kipindi kifupi kilichobakia.

Ushauri huo ulitolewa leo na Mtaalamu wa Uendelezaji Biashara nchini(Business Development Expert) ,Mtaturu Mkonongo wakati akizungumza mjini ambapo alisema kabla ya kuelekea uchaguzi mkuu mabadiliko kwenye nafasi za mawaziri unapaswa kuzingatia kwa umakini mkubwa ikiwemo uwajibika kwa watakaoteueliwa.



Mkonongo alisema anaamini waziri mpya wa Fedha na Uchumi atakayirithimikoba ya Dr.William Mgwimwa ataweza kuisaidia serikali katika kutekeleza kwa vitendo maamuzi halali ya kisiasa na kitaalamu kwa kuzipa kipaumbele sekta za kilimo,elimu na miundombinu ili kurahisisha kukua kwa uchumi wan chi.


   “Bila kuboreshwa elimu ya motto wa mkulima wa Tanzania ikiwemo kilimo cha mkulima wa kawaida wan chi hii kamwe hatutaweza kupata maendeleo endelevu ya rasilimali zetu “Alisema Mkonongo.


Mkonongo ambaye pia ni mjasiria mali wa kati alielezea mambo mengine  ambayo yangepaswa kufanyiwa kazi ipasavyo katika kipindi hiki kifupi kilichobakia ni kuendelea na uimarishwaji wa miundombinu ya barabara ambazo zitaweza kurahisisha utendaji wa wananchi na hivyo kupeleka kuwa na maisha bora.


Aidha aliwataka watendaji ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) katibuMkuu Abrahamani Kinana na katibu itikadi na uenezi Nape Nnauye wabaki kuwa washauri wa Rais Kikwete katika utekelezaji wa shughuli zake za kimaendeleo ndani na nje ya nchi.

Hata hivyo alimuomba Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama  Cha Mapinduzi asikie kilio cha watanzania kuhusu umuhimu wa mawaziri kukisaidia chama hicho kwa kufanya kazi wanazoagizwa kwa kuwajibika kwa nafasi walizonazo ili kuweza kuwatambua uzembe wao na kuufanyia kazi.


    “Viongozi watambue kuwa uzembe au uvivu wao utaigharimu serikali hivyo wahakikisha wanakuwa mstari wa mbele kulinda na kutetea maslahi ya chama na taifa kwa ujumla ili kuendana na kazi ya maendeleo kama ilivyokuwa kwa nchi nyengine duniani.


Akizungumzia suala la Rasimu ya Katiba,Mkonongo alisema wanachokiomba  bunge lijalo lipitishe serikali mbili ya Muungano na ya Zanzibar kama ilivyokuwa sasa ili katiba mpya itatue kero za siku nyingi za Muungao.


Hata hivyo alishauri kuwa mawaziri wasiwe wabunge ili waweze

kuwajibishwa mara moja pindi wanaposhindwa kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa kushindwa kuwapa maendeleo wananchi wao ikiwemo kutatua kero zao zinazowakabili.

No comments:

Post a Comment