Pages

Pages

Thursday, January 16, 2014

Ajali yaua watano kujeruhi wawili wilayani Handeni mkoani Tanga

Na Rajabu Athumani, Handeni
WATU wanne wamekufa papo hapo na mmoja hospitali katika ajali ya basi aina Noa ilitokea jana majira ya jioni katika Kitongoji cha Mtakuja kata ya Misima wilayani Handeni na kujeruhi wengine wawili.

Mmoja wa shuhuda wa ajali hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Rashidi alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kukatika kwa chuma kinajulikanacho kama propera shafti ambacho kilikatita na kusukuma gari pembeni na kupinduka zaidi ya mara tatu na kusababisha vifo hivyo na majeruhi.

Habari kutoka eneo la tukio zilieleza kuwa dereva wa gari hilo aliyejulikana kama Miraji Shabani(22) ametoroka baada ya ajali kutokea na hajulikani alipo hadi sasa na polisi wanaendelea kumtafuta kwa mahojianao.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Costantine Massawe alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa ni kweli gari yenye namba za usajili T493 AUH aina ya Noa na kuua watu wanne hapo hapo na mmoja hospitali baada ya kukatika chuma wanachoita propera shafti hali iliyosababisha kuuwa watu watano katika ya saba waliokuwa katika Noa hiyo.

Kamanda Massawe alisema kuwa Noa hiyo ilikuwa ikitokea Handeni mjini kuelekea Misma kilomita 16 kutoka mjini ikiwa na wanafamilia hao saba wakiwa humo kwaajili ya shughuli zao binafsi za kifamilia na haikuwa gari ya kibiashara.

Kamanda Massawe aliwataja marehemu wa ajali hiyo kuwa ni Juma Nyeri (90) mkazi wa Misima,Athumani Yusuph (45),Zahara Changogo,Mwajuma Mzimu na Zuberi Abdallah wote wakazi wa Suwa wilayani Handeni na majeruhi ni Hemedi Said ambae baada ya kupatiwa matibabu alipewa ruhusa na kurudi nyumbani pamoja na dereva ambae alishakimbia hiyo haijulikani kuwa ameumia kiasi gani..

No comments:

Post a Comment