Pages

Pages

Tuesday, January 21, 2014

Malinzi awazodoa Simba na Yanga



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
RAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi, amevipiga vijembe vilabu vya soka vya Simba na Yanga, kwa madai kuwa vinajiendesha kizamani kwa kutegemea ada ya uanachama, hivyo kukalia utajiri wao.


Rais wa TFF, Jamal Malinzi, pichani.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Malinzi alisema kuwa mfumo unaoendesha timu za Simba na Yanga ni mbaya na maendeleo kwao yatachelewa kupatikana na kubakia na majina yao.

Alisema huu si wakati wa kusubiria ada ndogo ya uanachama wakati mipango kabambe ikiwekwa inaweza kuzinufaisha timu hizo na kuondoka kwenye kutegemea mifuko ya watu wachache.

“Katika uongozi wetu huu lazima wanachama wetu wabadilike na kufanya vitu vyenye maana ili kuendeleza soka la Tanzania na kupiga hatua na kutoka hapa tulipokuwa sasa.

“Viongozi wanapaswa kutumia vizuri nafasi zao kwa kushirikiana na wanachama wao na wataalamu wao, ukizingatia kuwa zipo mbinu nzuri zenye tija, ukiwapo mpango wa hisa unaoweza kutajirisha timu zetu,” alisema.

Malinzi amerithi mikoba ya Rais wa TFF aliyemaliza muda wake, Leodgar Tenga, huku akiingia kwa mkwara mzito na mipango lukuki ya kuiletea maendeleo Tanzania katika sekta ya mpira wa miguu.

No comments:

Post a Comment