Pages

Pages

Tuesday, January 21, 2014

Kipingu afurahia vijana wa tenisi akitaka waendelezwe



Na Kambi Mbwana, Nadhani Sh 10,Ma
KOCHA wa timu ya Taifa ya tenisi Tanzania, Kyango Kipingu, amesema kwamba mipango ikiwekwa na ushirikiano kutoka kwa wadau wote wa michezo, tenisi itapiga hatua.

Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, Kipingu alisema kuwa ni vyema wadau na serikali ikakaa na kuliangalia kwa kina juhudi za kuendeleza mchezo wa tenisi.

Alisema kuwa vijana wengi wa Tanzania wanaonyesha shauku ya kutangaza vipaji vyao katika tasnia ya mchezo wa tenisi, hivyo ni wakati huu kuliwekea mkazo.
“Nashukuru kuona mara kwa mara vijana wetu wa Tanzania wanajituma uwanjani katika mashindano mbalimbali yanayofanyika ndani na nje ya nchi.

“Hapa kwetu katika mashindano ya Afrika yaliyomalizika mwishoni mwa wiki tulimaliza huku timu yetu ikishika nafasi ya pili, jambo ambalo linaonyesha namna gani wachezaji wapo,” alisema.
Hata hivyo, tenisi ni miongoni mwa michezo inayoonekana kuwa wanaocheza ni wale wanaojimudu kimaisha, jambo ambalo baadhi yao wanapinga.

No comments:

Post a Comment