Pages

Pages

Saturday, November 16, 2013

Wacheza shoo wajipanga kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha chama chao


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

KATIBU wa Mkoa wa Dar es Salaam wa Chama Cha Wacheza Shoo, Super Nyamwela, amesema wameamua kuanzisha chama chao ili kujipanga na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Nyamwela  pichani,  alisema kwamba wacheza sho siku zote wamekuwa wakiishi maisha ya kubangaiza huku wakiwa hawana maisha mazuri kutokana na kazi zao.

Alisema jambo hilo limewafanya waanzishe chama hicho kwa ajili ya kusaidiana na kukabiriana na changamoto zozote zinazokuja mbele yao katika tasnia ya muziki hapa nchini.

“Tumeanzisha chama cha wacheza shoo kwa ajili ya kuungana kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa mambo yetu yanakuwa mazuri na tunajipanga kwa lolote linaloweza kutokea katika kazi zetu,” alisema Nyamwela.

Super Nyamwela ni miongoni wacheza shoo wenye mvuto na kipaji cha aina yake, huku akiitumikia bendi ya Extra Bongo, chini ya Ally Choki, huku akifanikiwa kuunda kikosi imara cha kulishambulia jukwaa.

No comments:

Post a Comment