Pages

Pages

Saturday, November 16, 2013

Kikapu Tanga waomba msaada kuipeleka timu Mbeya


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

MABINGWA watetezi wa michuano ya Taifa ya kikapu (Taifa Cup) hawajathibitisha ushiriki wao katika michuano ya mwaka huu kutokana na kukabiriwa na ukata wa kifedha.


Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mpira wa kikapu mkoa wa Tanga (TRBA), Carlistus Zakaria, timu hiyo inahitaji kiasi cha Sh milioni 11, ili iweze kusafiri hadi mkoani Mbeya.


“Timu yetu ina wachezaji 24 Wavulana na Wasichana pamoja na viongozi wanane hivyo kufanya idadi ya watu 32, tunahitaji kiasi cha Sh mil 3.5 za nauli kuenda na kurudi, Sh mil 5.2 za chakula kwa siku zote tutakazokuwa Mbeya pamoja na Sh mil 8.8 za vifaa vya michezo na fedha za dharura.


“Tunaomba msaada kwa wadau wote wa michezo hususan wa mkoani Tanga ambao wenyewe walishuhudia na kutupongeza tulivyofanya vizuri katika mashindano hayo,” ilisema barua hiyo ya TRBA.

Kwa mujibu wa TRBA, mdau yoyote anaweza kuwasaidia kwa ajili ya kuweka kambi yao kwa kama maandalizi ya kushiriki mashindano hayo Novemba 30 hadi Disemba 8, huku wakiwataka wadau hao kuwachangia kwa kupitua akaunti ya benki namba 4172506984 NMB Bank (badaraka Branch).

No comments:

Post a Comment