Pages

Pages

Tuesday, November 12, 2013

Mapacha Watatu sasa hapatoshi Novemba 22

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

BENDI ya Mapacha Watatu, sasa inatarajia kufanya onyesho lake la kutimiza miaka minne tangu kuanzishwa kwake katika Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama, Novemba 22, kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki na kuonyesha uwezo wao kimuziki.

Mapacha Watatu pichani.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa bendi hiyo, Khamis Dacota, alisema kwamba awali walipanga kufanya onyesho hilo mwishoni mwa wiki hii, lakini wameamua kusogeza mbele.


Alisema kwamba onyesho hilo litakuwa la aina yake kutokana na dhamira yao ya kuonyesha burudani sahihi kutoka kwa wadau na mashabiki wao wa muziki wa dansi wanaoendelea kuwaunga mkono.

“Vijana wangu wanaendelea kujipanga kwa kuhakikisha kuwa wanatoa burudani za aina yake kwa mashabiki wao wanaowapenda, ukizingatia kuwa muziki kwao ni ajira,” alisema Dacota.


Bendi hiyo ipo chini ya Khalid Chokoraa, akiwa sambamba na Jose Mara, moja ya vijana wanaokubalika mno katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini, tangu walipojitoa katika bendi zao na kuunganisha nguvu Mapacha Watatu.

No comments:

Post a Comment