Pages

Pages

Monday, November 25, 2013

Juhudi za kukuza elimu Tanzania

Gavana wa Lions Club, katika nchi ya Tanzania na Uganda, Wilson Desanjo, akijumuika katika picha ya pamoja na viongozi wa Shule, Wanafunzi wa shule ya msingi ya Rau, pamoja na viongozi wa Klabu ya Lions Kibo Moshi na Diwani wa kata ya Rau, Peter Kimaro.
Gavana wa Lions Club, katika nchi ya Tanzania na Uganda, Wilson Desanjo, akisikiliza maelezo kutoka kwa mratibu wa Klabu ya Lions Kibo Moshi, Inderjeet Rehal "Nitu" (mwenye kilemba chekundu) kuhusu ujenzi wa majengo mbalimbali katika shule ya msingi Msandaka.
Gavana wa Lions Club, katika nchi ya Tanzania na Uganda, Wilson Desanjo, akisikiliza maelezo kutoka kwa mratibu wa Klabu ya Lions Kibo Moshi, Inderjeet Rehal "Nitu" (mwenye kilemba chekundu) kuhusu kompyuta zilizoko katika katika shule ya msingi Msandaka.
Gavana Desanjo akishirikiana na Mama Martha Msuya ambaye ni mke wa Marehemu Gavana Fadhili Msuya kuzindua, jengo la Choo katika shule ya msingi Msandaka. choo hicho kimejengwa kwa ufadhili wa ndugu za Marehemu Msuya kwa kushirikiana na Lions Kibo Moshi.
Gavana wa Lions Club, katika nchi ya Tanzania na Uganda, Wilson Desanjo, akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa jengo la Bweni ya wasichana katika shule ya Msingi ya Viziwi ya Msandaka, iliyoko katika manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro jana. wanaoshuhudia ni Gavana wa Lions Club, katika nchi ya Tanzania na Uganda, Wilson Desanjo (kulia) Mwenyekiti wa Lions Kibo Moshi, Joleon Johns (kulia) na Mratibu wa Klabu hiyo, Inderjeet Rehal.
Gavana wa Lions Club, katika nchi ya Tanzania na Uganda, Wilson Desanjo (kulia) akisaidiwa na Mwenyekiti wa Lions Kibo Moshi, Joleon Johns (kushoto) kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa jengo la Bweni ya wasichana katika shule ya Msingi ya Viziwi ya Msandaka, iliyoko katika manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro jana. picha na Fadhili Athumani.
Gavana wa Lions Club, katika nchi ya Tanzania na Uganda, Wilson Desanjo, akishiriki zoezi la upandaji miti katika shule ya msingi ya Viziwi ya Msandaka, Katika Manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment