Pages

Pages

Sunday, October 27, 2013

Yanga waitangazia hatari Mgambo JKT

NaKambi Mbwana, Dar es Salaam
TIMU ya Yanga, imeitangazia hali ya hatari Mgambo JKT, ikisema itahakikisha inaibuka na ushindi mnono katika mchezo huo uliopangwa kufanyika Jumanne ya Oktoba 29 katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Kocha msaidizi wa Yanga, Fredy Minziro.
Mechio hiyo inachezwa huku Yanga wakiwa na shauku ya kuibuka na ushindi huo ili iweze kujiweka pazuri katika patashika ya Ligi ya Tanzania Bara, ambapo katika mechi iliyopita, mabingwa hao watetezi waliibuka na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Rhino Rangers ya mjini Tabora.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Fredy Minziro, alisema kwamba timu yao imeanza mazoezi kwa ajili ya kujiwinda na Mgambo huku wakiwa na hamu ya kushinda dhidi ya Mgambo JKT.

Alisema kuwa kikosi chao chote kimeanza mazoezi makali kwa ajili ya mechi hiyo itakayokuwa na ushindani wa aina yake, kutokana na timu zote mbili kutaka kushinda  dhidi ya mwenzake, jambo ambalo kwa upande wa Yanga wanakabiliana nalo.
“Tumekusudia kushinda mechi tatu mfululizo ili tupate pointi 28 ambazo tunaamini tutakuwa tumemalizia mzunguuko wa kwanza wa ligi kw3a kuwa kileleni, hivyo lazima tufanikishee katika hilo ili tutimize kiu yetu.

“Ingawa tunajua mchezo huu utakuwa mgumu kupita kiasi, ila hatuna sababu ya kushindwa kufanya vyema kwakuwa lengo letu ni kutetea ubingwa wetu na lazima tuupate kwa kuhakikisha kuwa tunakuwa kitu kimoja na tunashinda kila mechi,” alisema.

Kwa mujibu wa Minziro, kikosi chao kinaendelea na mazoezi katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Luyola, ambapo lengo lao ni kuibuka na ushindi mnono katika mechi hiyo dhidi ya Mgambo JKT, Jumanne ijayo.

No comments:

Post a Comment