Pages

Pages

Wednesday, October 09, 2013

Vida aendelea kukaza msuri Bongo Fleva

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Pili Juma, maarufu kama Vida, amesema malengo yake ni kufanya kazi nzuri kwa ajili ya kuonyesha kipaji chake katika kona ya muziki wa kizazi kipya nchini.
                                                    Vida akiwa kwenye pozi.
Vida anayetamba na wimbo wake wa Baba Awena, huku akimshirikisha nyota wa muziki nchini, Linex, anatokea katika taasisi ya kukuza na kulea vipaji ya Tanzania House of Talent THT.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Vida alisema kuwa sanaa ya muziki kwake ni kipaji, hivyo anaamini malengo yake yatatimia kwa kuweka mkazo kwenye utendaji wake wa kazi.

Alisema kuwa japo anajua changamoto na ugumu uliopo katika tasnia hiyo, ila amejipanga vizuri kwa ajili ya kutimiza malengo yake katika tasnia ya muziki huo nchini.

“Nimekuwa nikifanya juhudi kubwa kuhakikisha kuwa mambo yangu yanakuwa mazuri pamoja na kuwapa burudani kamili wadau na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini.

“Najua ugumu uliopo lakini si sababu ya kunifanya nishindwe kuongeza bidii na kukuza harakati zangu katika tasnia hiyo, ukizingatia kuwa ndio malengo yangu ya kutangaza muziki huu,” alisema Vida.

Vida ni miongoni mwa wasanii mahiri wa kike wanaotokea katika taasisi hiyo ya THT yenye vichwa kadhaa, akiwamo Recho, Mwasiti, Linah na wengineo wanaofanya vizuri katika muziki huo.

No comments:

Post a Comment